Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho, Mukwala katika vita nzito

AUCHO Pict

Muktasari:

  • Wengine wanaowania tuzo hiyo mbali na Aucho na Mukwala wanaocheza Ligi Kuu Bara, ni Bevis Mugabi wa Anorthosis Famagusta ya Cyprus, Elio Capradossi wa SC Cittadella ya Italia na Rogers Mato wa FK Vardar iliyopo huko Skopje, Macedonia Kaskazini.

VITA ya nyota wawili wa Yanga na Simba, kiungo Khalid Aucho na mshambuliaji Steven Mukwala imehamia Uganda, baada ya kuteuliwa kuwania tuzo za Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), katika kipengele cha Mwanasoka Bora Anayecheza nje ya nchi.

Wengine wanaowania tuzo hiyo mbali na Aucho na Mukwala wanaocheza Ligi Kuu Bara, ni Bevis Mugabi wa Anorthosis Famagusta ya Cyprus, Elio Capradossi wa SC Cittadella ya Italia na Rogers Mato wa FK Vardar iliyopo huko Skopje, Macedonia Kaskazini.

Kiwango bora cha nyota hao msimu huu katika Ligi Kuu Bara, kinawafanya kuingia katika tuzo hizo ambapo watakabiliana na mastaa wengine kutoka nje ya mipaka hiyo, huku kiu ya mashabiki ni kuona ni yupi ataibuka kidedea kati ya hao wawili tu.

Aucho aliyejiunga na Yanga Septemba 8, 2021, akitokea Misr Lel Makkasa ya Misri, amekuwa nguzo muhimu ya timu hiyo, huku akiiwezesha kutwaa mataji mbalimbali yakiwemo ya Ligi Kuu mara tatu mfululizo sawa na Kombe la Shirikisho la (FA).

Kwa upande wa Mukwala ameonyesha kiwango bora hadi sasa akiwa na kikosi hicho cha Msimbazi katika mashindano mbalimbali akiiwezesha timu yake kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, tangu ajiunge nacho msimu huu, akitokea Asante Kotoko ya Ghana aliyofanya nayo pia vizuri kwa msimu uliopita.

Nyota huyo aliyetamba na timu mbalimbali zikiwamo za Edgars, Buleemezi, Ssingo, Vipers, Maroons FC na Kampala City, amekuwa katika kiwango bora, licha ya changamoto ya ushindani wa kuwania nafasi katika kikosi hicho.

Mukwala hadi sasa amefunga mabao 11 ya Ligi Kuu, akizidiwa bao moja na mshambuliaji wenzie wa kikosi hicho, Leonel Ateba mwenye 12, ingawa amezidiwa manne na kiungo mshambuliaji pia wa timu hiyo, Jean Charles Ahoua anayeongoza na 15.

Nyota huyo ametua Simba huku akikumbukwa zaidi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 14 akiwa na kikosi cha Asante Kotoko, nyuma ya kinara mshambuliaji wa Berekum Chelsea, Stephen Amankonah aliyefunga mabao 16.

Tuzo nyingine zinazowaniwa ni Mwanasoka Bora wa kiume ambapo wanaoshindania ni Denis Omedi na Jude Ssemugabi wanaochezea Kitara, Allan Okello (Vipers), huku wengine ni Ssekiganda Ronald na Kakande Jonah Patrick wanaoichezea SC Villa.

Katika tuzo za Mwanasoka Bora wa Kike wanaowania ni Agnes Nabukenya (Kawempe Muslim Ladies), Daisy Nakaziro, Nalugya Shamirah na Nandede Zainah wanaochezea kikosi cha Kampala Queens na Kabusobozi Resty anayechezea Lady Doves.

Kocha Bora wa Kiume wanaochuana ni Mbalangu Hussein (NEC FC), Ssenyondo Brian (U-17), Dusan Stojanovic wa SC Villa, huku kwa timu za kike ni Frank Anyau (Amus College), Issa Hassan (She Corporate LFC) na Ayub Khalifah Kiyinji wa Kawempe Muslim LFC).

Mwanasoka Bora anayeinukia wanaowania tuzo hizo ni Okello Richard (BUL), Jara Brian (KCCA) na Bogere James wa Masaka Sunshine, huku soka la ufukweni ni Kasibante Edward wa Buganda Royal na Lule Paul (Kampala).