Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viungo Kagera wamkuna Mauya

MSIMU uliopita Kagera Sugar ni moja ya timu za Ligi Kuu Bara zilizokuwa na safu mahiri ya kiungo ikiongozwa na nyota Zawadi Mauya aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu na kupitia gazeti hili Mauya amewapongeza viungo wa timu hiyo kwa sasa na kuwatakia mema.

Mauya anayesifika kwa kukaba na kupiga pasi zenye macho ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali kuwa anaionaje Kagera ya sasa hususan eneo la kiungo tangu aondoke klabuni hapo.

“Wako vizuri, akiondoka mchezaji yeyote kwenye timu kuna baadhi ya mambo yatabadilika na hivyo ndivyo imetokea kwa Kagera, mimi wakati niko pale nilijitahidi kuipambania timu kwa uwezo wangu nikishirikiana na wenzangu, nilivyoondoka alihitajika mtu wa kuziba pengo langu na wengine walioondoka.

“Wakati ligi inaanza muunganiko wao ulikuwa bado hauko vizuri lakini kadri siku zilivyokwenda walipambana na kufiti kwenye mfumo, nawapongeza kwa hilo maana moja ya sifa za timu ile ni kucheza soka eneo la kiungo na sasa wanafanya hivyo, hakuna anayetia shaka kwa uwezo wao,” alisema Mauya.

Pia Muaya alizungumzia maisha yake ya sasa ndani ya Yanga na kuweka wazi anafurahia kuwa katika timu hiyo na akili, nguvu na maarifa yote ameyaweka kwa vinara hao wa Ligi Kuu mpaka sasa.

“Maisha ya Yanga ni mzuri pia ni tofauti na Kagera, kwa sasa nafurahia kuwa hapa na najitoa kwa kadri ninavyoweza kuitumikia timu hii, wachezaji wote tuna umoja na mshikamano pia kwa viongozi wetu jambo linalomfanya kila mmoja wetu kujivunia kucheza kikosini hapa,” alisema.