Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Yanga wapewa siku saba

KOCHA wa mazoezi wa viungo Yanga, Edem Mortotsi amekiangalia kikosi hicho na kisha kuwafungukia mastaa wake akiyataja mambo mawili aliyoyashtukia na anahitaji wiki moja kuhakikisha mambo yanabadilika haraka katika kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mortotsi ambaye ni raia wa Ghana alisema alichoshtukia ni wachezaji wake wameanza kuwa fiti, lakini bado hawajafikia kiwango anachotaka ili waweze kutisha zaidi.

Mortotsi alisema kwa sasa anawaona wachezaji wake kufikia asilimia 80 ya ufiti, lakini ndani ya wiki moja watakamilisha 100 baada ya wote kujiunga na timu hiyo.

“Bado kidogo nawaona wanaimarika taratibu naweza kusema sasa wako kwenye asilimia 75-80 lakini bado hawajafikia ambako nataka wangalie baada ya siku saba zijazo tu utagundua ninachosema,” alisema Mortotsi.

“Changamoto ndogo ambayo tumekutana nayo ni wachezaji kuwa katika makundi mawili tofauti kuna waliokuwa nasi lakini kuna wengine walikuwa katika timu za taifa wamerudi wako fiti lakini lazima wachezaji uwatengeneze wakiwa pamoja.

Aidha Kiungo huyo wa zamani mchezeshaji aligusia pia ubora wa viungo wa timu hiyo akisema wala hajaona wasiwasi na kwamba amegundua kuna vipaji bora ambavyo sasa vinatakiwa kupewa mbinu.

“Viungo nawaona wako ambao wanaweza kutusaidia sana, wanaubunifu lakini pia wana njaa ya mafanikio kitu muhimu sasa ni kuwaongezea mbinu, nilikuwa nacheza nafasi hiyo nitashauriana na kocha mkuu lakini hata wao wenyewe nitakuwa nawaongezea kitu tukiwa mazoezini,” alisema.