Vita ya BDL kurudi Julai 10

Muktasari:
- Ratiba iliyotolewa na kamishina wa ufundi na mashindano wa BDL, Haleluya Kavalambi, imeonyesha mchezo wa kwan-za utakuwa kati ya Kurasini Divas na DB Troncatti, ukifuatiwa na mchezo kati ya Pazi Queens na Reel Dream.
BAADA ya kukosa kuangalia utamu wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kwa wiki mbili, ligi hiyo itaendelea tena Julai 10, kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga.
Ratiba iliyotolewa na kamishina wa ufundi na mashindano wa BDL, Haleluya Kavalambi, imeonyesha mchezo wa kwan-za utakuwa kati ya Kurasini Divas na DB Troncatti, ukifuatiwa na mchezo kati ya Pazi Queens na Reel Dream.
Baadaye timu ya Srelio itacheza dhidi ya Kurasini Heat na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Stein Warriors na DB Or-atory.
Kati ya michezo itakayochezwa siku hiyo, mchezo kati ya timu ya Stein Warriors na DB Oratory, ndiyo unaosubiriwa na wapenzi wengi wa kikapu.
Mchezo huo uliogusa wapenzi hao, umetokana na kiwango kizuri walichoonyesha katika michezo yao iliyopita.
Timu ya Stein Warriors inayoongoza kuwa na wapenzi wengi katika Ligi hiyo, inashika nafasi ya 4 kwa pointi 14, katika msimamo wa Ligi hiyo.
Baadhi ya mchezo iliyocheza, iliishinda timu Srelio kwa pointi 71-61, Savio pointi 93-74 baadaye ikafungwa na UDSM kwa pointi 69-65.
Kwa upande wa timu ya DB Oratory inayoshika nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi hiyo kwa pointi 12, iliifunga Srelio kwa pointi 76-72, Savio pointi 75-76 na Chui pointi 66-58.
Michezo mingine iliifunga Mchenga Star kwa pointi 75-47, KIUT pointi 70-62 baadaye ikafungwa na UDSM kwa pointi 62-57 na Pazi pointi 77-49.
Timu ya Stein Warriors inajivunia wachezaji wake Jonas Mushi, Mwalimu Heri, Evance Davies na Brian Mramba huku DB Oratory ikijivunia na Isaya William, Oswald Bera na Hassan Kabanda.
Ligi itaendelea siku ya Julai 11, Kigamboni Queens ikiikabili Polisi Stars, Tausi Royals vs Ukonga Queens, Dar City vs KIUT na Pazi itakayoivaa Mchenga Star.