Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wallace Karia mgombea pekee Urais TFF

UCHAGUZI Pict

Muktasari:

  • Akitangaza ripoti ya usahili wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF Wakili Kiomoni Kibamba, amesema Karia ndiye mgombea pekee aliyekidhi vigezo na kwa mujibu wa Kanuni na kama kuna mtu anapingamizi bado ana nafasi ya kufanya hivyo .

Kamati ya Uchaguzi ya TFF Imewang'oa wagombea watano wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kubaki na jina moja la Wallace Karia anayetetea kiti hicho.

Akitangaza ripoti ya usahili wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF Wakili Kiomoni Kibamba, amesema Karia ndiye mgombea pekee aliyekidhi vigezo na kwa mujibu wa Kanuni na kama kuna mtu anapingamizi bado ana nafasi ya kufanya hivyo .

Kibamba amesema wagombea wengine wanne kati ya sita wamekosa sifa za kukidhi kanuni za uchaguzi huku mgombea mmoja akishindwa kutokea kwenye usahili.

"Kwenye nafasi ya urais kulikuwa na wagombea sita, mmoja hakutokea kwenye usahili na wengine wanne hawakukidhi matakwa ya kikanuni, mgombea mmoja amekidhi matakwa yote ya kikanuni na tumempitisha ambaye ni Wallace Karia,"amesema Kibamba.

Kibamba ameeleza kuwa kwenye nafasi ya wagombea wa nafasi ya ujumbe kulikuwa na wagombea 19 ambapo 17 walihudhuria usahili, saba wamekosa vigezo na kumi wamepitishwa kuendelea na mchakato wa uchaguzi katika hatua inayofuata.

Hata hivyo, Kibamba amesema wagombea ambao wamekosa sifa na kukatwa, wana nafasi ya kwenda kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya uchaguzi endapo wataona hawajatendewa haki.

"Sisi ni kamati ya uchaguzi na ni binadamu inawezekana wapo ambao wataona wameonewa wana nafasi ya kwenda kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi, wakiturudishia jina lake, sisi hatuna shida, tutalipokea na kuendelea na uchaguzi.

"Kutakuwa na siku sita za kukata rufaa na sisi Kamati ya Uchaguzi tutapokea orodha kamili ya wagombea kutoka kwa Kamati ya rufaa ili tuendelee na hatua inayofuata.

Wagombea sita ambao walichukua fomu ya kugombea urais wa TFF ni Wallace Karia, Richard Shija, Mshindo Msolwa, Ally Mayai, Mustapha Himba na Ally Thabit Mbingo.