Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Prisons, Mbeya City kupigwa pini Sokoine

SOKOINE Pict

Muktasari:

  • Uwanja huo pekee mkoani Mbeya ndio hutumika mara kadhaa kwa timu za jijini humo kufanya mazoezi na mechi nyingine za mashindano ikiwa ni pamoja na za Ligi Kuu, Championship na First League.

MENEJA wa Uwanja wa Sokoine, Modestus Mwaluka amesema licha ya rekodi aliyoweka ya kutofungwa kwa uwanja huo, ataendelea kuwa mkali kwa timu zinazotumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.

Uwanja huo pekee mkoani Mbeya ndio hutumika mara kadhaa kwa timu za jijini humo kufanya mazoezi na mechi nyingine za mashindano ikiwa ni pamoja na za Ligi Kuu, Championship na First League.

Katika msimu uliomalizika hivi karibuni, uwanja huo mkongwe haukuwa kati ya viwanja vilivyofungiwa, huku meneja huyo akibeba tuzo ya mwezi Septemba kwa utunzaji bora.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwaluka alisema utunzaji wa uwanja ni gharama akiwashukuru wamiliki (Chama cha Mapinduzi) kwa sapoti waliyotoa kwa muda wote.

Amesema pamoja na furaha yake kuongezeka timu za Ligi Kuu msimu ujao ikiwa ni Tanzania Prisons na Mbeya City, amesema atakuwa mkali kwa yeyote atakayetumia uwanja huo kwa mazoezi.

“Kwa siku tatu inatumika Sh 100,000 kwa ajili ya maji wakati wa kiangazi, lakini kipindi cha mvua inahitajika mchanga wa mtoni hizo zote ni gharama, kwa maana hiyo nitaendelea kuwa mkali.

“TFF inashauri na kuelekeza kila timu iwe na uwanja wake wa mazoezi, hivyo ili kuweza kulinda heshima na kibarua changu lazima nilinde vyema uwanja huu na kuutunza,” alisema Mwaluka.