VIDEO: Azam yajificha Moro kuikabiri Mtibwa Sugar

Muktasari:
Azam inakwenda katika mchezo huo ikiwa kumbukumbu ya kutolewa na Mtibwa Sugar katika robo fainali ya Kombe la FA
Morogoro. Azam FC imeweka kambi ya muda mjini Morogoro jana jioni ikijiandaa na mchezo wake kesho Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Tuliani.
Azam kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi Idd Cheche baada ya kocha wake mkuu Aristica Cioaba kusimamishwa na kamati ya nidhamu kwa muda.
Cheche alisema mchezo wao utakuwa mgumu na kuvutia, lakini anaamini atatoka na ushindi au pointi ya aina yoyote.
"Siyo kama kocha mkuu akiwa hayupo basi ndio kila kitu kinaharibika, lakini hapa kinachofanyika chote ni kuhakikisha kwamba programu na mifumo ya mwalimu inaendelea, tunafahamiana vizuri na Mtibwa mchezo utakuwa mzuri," alisema Cheche.