Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti ya jeraha la Dube yashtua

DUBE Pict

Muktasari:

  • Timu hizo zitavaana Juni 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika pambano hilo la marudiano la Ligi Kuu kwa msimu huu, huku kila moja ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kubeba ubingwa kutokana na kutofautiana pointi moja, Yanga ikiwa na 76 dhidi ya 75 za Simba kila moja ikicheza mechi 28.

MASHABIKI wa soka kwa sasa wanahesabu siku kabla ya kushuhudia pambano la Dabi ya Kariakoo lililopangwa kupigwa Juni 25 baada ya kuahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15, kuna taarifa ambayo huenda isiwe nzuri kwa mashabiki wa Yanga.


Timu hizo zitavaana Juni 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika pambano hilo la marudiano la Ligi Kuu kwa msimu huu, huku kila moja ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kubeba ubingwa kutokana na kutofautiana pointi moja, Yanga ikiwa na 76 dhidi ya 75 za Simba kila moja ikicheza mechi 28.


Hata hivyo, taarifa ni kwamba imebainika kuwa mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube aliyecheza kwa dakika 22 tu jana katika pambano dhidi ya Tanzania Prisons na kutolewa kutokana na kuumia, yupo hatihati kuicheza Dabi.

Dube alitolewa uwanjani dakika 22 katika ushindi wa mabao 5-0, mawili yakiwekwa kimiani na Pacome Zouzoua, Mudathri Yahya, Israel Mwenda na Clatous Chama aliyeingia badala ya straika huyo Mzimbabwe amepata maumivu ya paja.

Daktari wa timu hiyo, Moses Etutu amesema Dube aliumia nyama za paja upande wa kushoto kwa uchunguzi wa awali walioufanya.

"Jana bahati mbaya akiwa anajiribu kuruka ili kuupiga kichwa alipata shida hiyo katika nyama za paja kwa uchunguzi tuliufanya nyama za pacha zimevutika kwa kiasi kikubwa hadi kumsababishia maumivu makali," amesema Dk Etutu na kuongeza;

"Tumemwanzishia matibabu ya hatua ya kwanza anaendelea vizuri kwa siku nzima ya jana na leo tunategemea ataanza vipimo zaidi tukirejea Dar es Salaam."

Etutu alisema vipimo zaidi vitakavyofanyika kesho ndio vitatoa taswira ya jeraha alilolipata litamuweka nje ya uwanja kwa muda gani kabla ya mechi mbili za ligi zilizo mbele yao na mchezo mmoja wa fainali Kombe la Shirikisho.

''Kwa sasa anaendelea vizuri na tumemfanyia matibabu ya awali ambayo hayategemei vipimo na anaonyesha kuwa katika hali nzuri tunategemea mambo yataenda vizuri atarejea kabla ya mechi zilizo mbele yetu."

Yanga ina mechi Jumapili hii dhidi ya Dodoma Jiji baada ya hapo itavaana na Simba Juni 25 na kucheza mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars siku ya Juni 29.

Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu, mchezaji mwenye maumivu ya nyama za paja za nyuma Harmstring bila ya kuchanika (Mild strain ) anaweza kupona ndani ya muda wa wiki 1-3 kwa kupumzika kuwekewa barafu na mazoezi mepesi ya kurejesha nguvu na tiba ya mwili tu.

Kwa daraja la pili (moderate strain) inayohusika kuchanika kiasi inayoambatana na maumivu ya kati, kuvimba na kumfanya mchezaji apate ugumu wa kutembea au kukimbi tiba yake ili apone inachukua wiki 4-8 ikiambatana na tiba ya mwili (physiotherapy) na kurejea polepole kwa mazoezi.

Kwa daraja la tatu (Severe strain or complete tear) inayosababisha msuli kuchanika kabisa ikiambatana na maumivu makali na ikiwa na michubuko au damu ndani ya ngozi, huchukua miezi mitatu au zaodo na wakati mwingine huhitaji upasuaji.