USM Alger yabeba CAF Super Cup ikiichapa Al Ahly

USM Alger imetwaa taji la CAF Super Cup ikiwachapa vigogo wa soka la Afrika mara 11, Al Ahly ya Misri kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa King Fahd nchini Saudi Arabia.
Fainali ya CAF Super Cup imewakutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly na wa Kombe la Shirikisho USM Alger kwa msimu uliopita.
USM Alger ilitwaa taji hilo la kwanza katika historia yao katika iwanja wao wa nyumbani licha ya kupoteza mchezo huo 1-0 dhidi ya Yanga kwa bao la ugenini baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
USM Alger inakuwa klabu ya pili nchini Algeria kushinda kombe hilo baada ya Wifak Setif mwaka 2015.
Vigogo Al Ahly iliwatoa mabingwa watetezi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca kwa ushindi wa mabao 3-2.