Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unaweza kupigwa 8-2, ila kawaida matokeo ni 1-0 tu

Muktasari:

Hata hivyo, mchezaji bora kuliko wote wa Crystal Palace ya England ni Wilfred Zaha lakini mpiga penalti wao ni Luka Milivojevic. Kwa hiyo si lazima kwa nyota wa klabu kuwa lazima ndiyo awe mpiga penalti.

KATIKA mchezo wa mpira wa miguu, yamewahi kutokea matokeo ya kushangaza yaliyowaacha vinywa wazi wapenzi wa mchezo huo. Manchester United imewahi kufungwa magoli sita na wapinzani wake Manchester City.

Wao Man United wenyewe wamewahi kuwafunga Arsenal magoli nane. Yanga ya Tanzania imewahi kufungwa magoli sita na Simba.

Imewahi kutokea na itaendelea kutokea. Hata hivyo, tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba matokeo ya wastani kwa mechi nyingi zilizopata kuchezwa huwa ni 1-0. Kwa hiyo, mara nyingi zaidi, mechi ya soka huisha kwa matokeo hayo.

Hayo si maneno yangu bali ni utafiti uliofanywa kwa kuangalia maelfu ya mechi zilizowahi kuchezwa katika ligi mbalimbali duniani.

Kwa sababu hiyo basi, inapotokea pigo laa adhabu ya penalti, mara nyingi kazi hiyo imekuwa ikiachwa kwa mchezaji ambaye amekuwa na uhakika wa kufunga kuliko wengine katika timu.

Penalti hiyo moja inaweza kuamua nani ashinde au ashindwe mechi. Ndiyo sababu, si ajabu kwamba katika dunia ya kisasa, kila timu kubwa duniani inajua kwamba inapotokea penalti katika sekunde ya mwisho ya dakika ya mwisho ya mechi, ni nani ambaye atapewa jukumu hilo.

Kila mchezaji ana uwezo wa kupiga na kufunga penalti; kwanza si kitu kikubwa sana. Lakini kwenye mashindano, hili ni suala la weledi na ndiyo sababu aliye bora ndiye hupewa nafasi.

Hutokea kwamba katika baadhi ya timu, mchezaji bora kuliko wengine ndiye pia huwa mpiga penalti namba moja. Tunaliona hili kwa Barcelona na Lionel Messi au Cristiano Ronaldo na Real Madrid au na Juventus kwa sasa.

Hata hivyo, mchezaji bora kuliko wote wa Crystal Palace ya England ni Wilfred Zaha lakini mpiga penalti wao ni Luka Milivojevic. Kwa hiyo si lazima kwa nyota wa klabu kuwa lazima ndiyo awe mpiga penalti.

Luis Suarez alikuwa mchezaji bora wa Liverpool, lakini mpiga penalti alikuwa ni Steven Gerrard. Aliyepata kuwa Meneja wa Liverpool, Gerrard Houllier, alizungumzia umahiri wa nahodha wake kwa kusema: “Steven Gerrard huwa anapeleka mpira pale anapotaka uende. Hana mfanowe kwenye hilo”.

Wakati akiwa Chelsea, Frank Lampard ndiye aliyekuwa mpiga penalti; mbele ya nyota wengine aliokuwa nao kama vile Didier Drogba, John Terry, Michael Ballack na wengineo ambao nao walikuwa wapiga penalti wazuri tu.

Tofauti na wenzake, Lampard alikuwa akibaki mazoezini peke yake na makipa wa akiba wa Chelsea akifanya mazoezi ya kupiga mipira iliyokufa –zoezi likiendelea muda mrefu baada ya kumalizika kwa mazoezi rasmi ya timu yake.

James Milner wa Liverpool ndiye mpiga penalti namba moja kwa sasa kwa timu yake hiyo. Kwa maelezo yake, anasema suala la upigaji penalti linachukua muda mrefu kuwa mahiri. Linahitaji uwezo wa kuzuia hisia zozote. Wewe unakwenda zako pale, unapiga penalti na halafu mpira unakwenda wavuni. Iwe dakika ya kwanza ya mchezo au dakika ya tisini.

Milner anasema hufanya uamuzi wa ni upande upi atapiga penalti yake siku moja kabla ya mechi. Kwa hiyo ikitokea tu penalti, anajua kama ataipiga katikati, kulia au kushoto kwa goli. Hii ndiyo saikolojia ya penalti.

Nimetoa historia yote hiyo kwa sababu wiki chache zijazo, Tanzania itakuwa inashiriki katika mashindano ya Kombe la Afrika kule nchini Misri. Ni muhimu sana kwamba benchi la ufundi likawa limemuandaa mtu wa kupiga penalti mashindano hayo yakianza.

Namna pekee ya kumjua nani ni mkali wao ni kwenye mazoezi tu. Wachezaji na benchi la ufundi watakuwa wanajua nani anastahili nafasi hiyo. Kama ukiniuliza mimi, nataka kuamini kwamba mtu anayestahili ni Erasto Nyoni.

Ni mchezaji mwandamizi ambaye ana uhakika wa kuanza mechi, ana uzoefu wa kupiga penalti zenye presha (Burkina Fasso zaidi ya miaka kumi iliyopita na majuzi dhidi ya Uganda pale Uwanja wa Taifa) na wenzake tayari wanamkubali. John Bocco ni mpigaji mzuri pia kama ilivyo kwa Mbwana Samatta. Hukohuko mazoezini watajua nani anastahili kuwa namba mbili na namba tatu.

Vyovyote itakavyokuwa, hatuwezi kwenda Misri wakati hatujui nani ni wa kwanza dhidi ya wenzake linapokuja suala la upigaji penalti. Tusisahau kitu kimoja; matokeo ya kawaida ni 1-0. Nafasi ikipatikana,.