Uhuru Selamani atuhumiwa kubaka

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili mchezaji wa zamani, Uhuru Selemani Mwambugu umeielezea Mahakama ya Wilaya ya Temeke jinsi alivyombaka mtoto wa kike ambaye ni ndugu yake.

Wakili wa Serikali Gace Lwila akimsomea maelezo ya awali  mbele ya Hakimu Mfawidhi, Aziza Mbadjo alidai Aprili 13, 2021 maeneo ya Chang'ombe Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam mtoto huyo akiwa nyumbani kwao alitembelewa na ndugu yake ambaye mshtakiwa Mwambugu

Lwila alidai kuwa mshtakiwa huyo baada ya kufika nyumbani kwa mtoto huyo akamuuliza  yupo na nani  ndipo akamjibu  yupo peke yake.

Alidai wakati huo mtoto huyo alikiwa amevaa kanga ndipo akamkaribisha ndani  alipoingia alimlazimisha kwa nguvu na kuanza kumbaka.

"Alipomaliza kumfanyia kitendo hicho alimwambia asimweleze mtu yeyote akisema atamfanyia kitu kibaya," alidai Lwila.

Lwila alidai baada ya kufanyiwa kitendo hicho alimwambia dada yake ndipo wakaenda kituo cha polisi cha Chang'ombe kutoa taarifa ambapo walipewa fomu ya matibabu(PF3).

Alidai baadaye walienda hospitali na majibu ya daktari yalipotoka ikabainika ameingiliwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mbadjo aliahirisha shauri hilo had Machi 28, 2022 kwa ajili ya ushahidi.

Katika kesi ya msingi April 13, 2021 maeneo ya  maeneo ya Chang'ombe Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam alimbaka mtoto wa kike.