Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshabalala amkaribisha upya Ajibu Simba

Muktasari:

Beki wa pembeni na nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amemkaribisha Ibrahim Ajibu.

Dar es Salaam. Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amemkaribisha kwa furaha mshambuliaji Ibrahim Ajibu aliyetambulishwa na kikosi hicho jana Jumatano.

Tshabalala nahodha msaidizi wa Simba amemkaribisha kutokana na ukaribu wake na Ajibu ndani na nje ya uwanja.

Ajibu amesajiliwa na Simba ikiwa ni mara ya pili baada ya kuachana nao miaka miwili iliyopita alipojiunga na Yanga.

Tshabalala alisema: "Karibu kwa mara nyingine staa Ibrahim Ajibu."

Tshabalala ataungana na Ajibu wakati wa maandalizi ya Ligi Kuu Bara ambapo Simba inatarajiwa kwenda Afrika Kusini.

Tshabalala alikuwa pamoja na kikosi cha Taifa Stars wakati Ajibu ni miongoni mwa wachezaji wachache waliokuwa wameachwa Dar es Salaam dakika za mwisho kabla ya Taifa Stars kwenda Misri.