Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF kufuatilia madai upulizaji dawa viwanjani

Muktasari:

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kasema suala hilo wanaliwekea mkazo kutokana na kuharibu taswira ya soka nchini.

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limekerwa na madai ya upulizwaji dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye viwanja mbalimbali vinavyotumika kwa ajili ya mechi.

 

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kasema suala hilo wanaliwekea mkazo kutokana na kuharibu taswira ya soka nchini.

 

Kumekuwepo na malalamiko kadhaa kwa baadhi ya timu kushindwa kuingia kwenye vyumba hivyo wakidai vimepulizwa dawa zinazoweza kuwadhuru wachezaji wao kiafya na kushindwa kucheza mpira wakati wa mechi za mashindano tofauti ikiwemo Ligi Kuu Bara.

 

Kidao alisema matukio ya timu za ligi kuu kuhusishwa kufanya vitu vya ovyo vyumbani wanavifuatilia kupitia kamera na kama wakigundulika watawachukulia hatùa.

 

"Uzuri viwanja vyote ambavyo vinalalamikiwa kuna kamera kwahiyo tutafuatilia na kama tukikuta matukio hayo basi timu mwenyeji itachukuliwa hatua," alisema.

 

Akizungumzia upande wa uwanja alisema anachotambua hakuna timu inayomiliki uwanja katika viwanja vinavyolalamikiwa zaidi ya wote kukabidhiwa funguo asubuhi hivyo matukio kama hayo lazima yafuatiliwe kwa umakini.

 

"Sio mpira tu wa nchi unaoharibiwa bali hadi taswira ya nchi inaharibika na hatupo tayari kuona jambo hili likitokea, kama watu wanawekewa hivyo vitu inashangaza na nipo katikati katika kukataa au kukubali kwasababu kama unapewa funguo na unakaa humo ndani kuanzia saa 12 asubuhi mpaka muda wa mechi mbona hawadhuriki wanaokaa?, " alisema Kidao.

 

Aliongeza kwa kusema kama wakifuatilia na kuona matukio hayo kwenye kamera basi hata uwanja itabidi ufungiwe kutokana na kuruhusu mambo hayo.