TETESI ZA USAJILI BONGO: Sadio Kanoute, JS Kabylie bado kidogo tu

Muktasari:
- Inadaiwa kuwa, Kocha Abdelhak Benchikha aliyefanya kazi na Putin wakiwa Msimbazi ndiye aliyetoa pendekezo la kiungo huyo wa kimataifa wa Mali asajiliwe katika timu hiyo.
KIUNGO mkabaji aliyetemwa na Simba hivi karibuni, Sadio Kanoute 'Putin' yupo mbioni kutua klabu ya Ligi Kuu ya Algeria, JS Kabylie.
Inadaiwa kuwa, Kocha Abdelhak Benchikha aliyefanya kazi na Putin wakiwa Msimbazi ndiye aliyetoa pendekezo la kiungo huyo wa kimataifa wa Mali asajiliwe katika timu hiyo.
Duru za kispoti zinadai kwamba mazungumzo ya menejimenti ya mchezaji huyo na JS Kabylie yanaendelea vyema na muda wowote Putin ataungana tena na Benchikha katika timu hiyo.
SADIO KANOUTE
Kuzaliwa: Okt 21, 1996
Mahali: Bamako
Nchi: Mali
Urefu: Mita 1.86
Klabu: Huru
Nafasi: Kiungo Mkabaji
Alikopita: Stade Malien, Al Ahli Benghazi na Simba