Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo Warriors waahidi Ubingwa Canaf 2021

Muktasari:

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa watu wenye ulemavu 'Tembo warriors' imeahidi kutwaa ubingwa wa mashindano ya Bara la Africa ya soka kwa watu wenye ulemavu 'Canaf' baada ya kutiga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa watu wenye ulemavu 'Tembo warriors' imeahidi kutwaa ubingwa wa mashindano ya Bara la Africa ya soka kwa watu wenye ulemavu 'Canaf' baada ya kutiga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Tembo Warriors imefanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya kuwaondosha timu ya taifa ya Cameroon katika hatua ya robo fainali kwa kipigo cha mabao 5-1 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam

Tembo Warriors ambao ndio mwenyeji wa mashindano hayo walifanikiwa kuanza vyema safari yao ya kutwaa ubingwa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Morocco mabao 2-1 katika mechi ya Ufunguzi ya michuano hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti kocha wa Tembo Warriors Salvatory Edward alisema kua msimuu wamejipanga kuakikisha kombe linabaki hapa nchini.

"Kiujumla mashindano ni magumu kwani kila timu imekuja kwaajili ya kucheza na kutwaa ubingwa hivyo tunapaswa kuongeza umakini katika kila mechi tunayocheza ili tupate matokea mazuri"

"Wachezaji wote wapo katika hali nzuri baada ya mchezo wa robo fainali na kila mchezaji anaonekana kua na kiu ya kutaka kufanya makubwa"alisema Salvatory

Kwa upande wa Nahodha wa Tembo Warriors Juma Kidevu ameliambia Mwanaspoti kua uwezo wanao na nguvu wanazo zakulibakisha kombe hapa nchini kwani wao Ndio wenyeji.


Wachezaji waipogeza Serikali

Mshambuliaji wa timu hiyo Alfan Kiyanga alisema kua wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani wamekua pamoja nao na kuhakikisha kua hawakumbani na changamoto yoyote itakayowapotezea molali ya mashindo.

"Tuna deni kubwa kwa taifa letu kwani wamefanya juhudu kuakikisha tunafika hapa tulipofika sasa na bila wao kutusapoti nafikiri tungekumbana na changamoto mbalimbali hivyo tunawashukuru sana"alisema Kiyanga