Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yapania Kombe la Dunia

Tanzania yapania Kombe la Dunia

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya soka kwa watu wenyewe ulemavu ‘Tembo Warriors’ wamepania makubwa kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa soka la walemavu Oktoba mwakani, nchini Uturuki 2022.

Wakizungumza na Mwanaspoti baada ya kuwashushia kipigo cha mabao 5-0 Cameroon katika mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa walisema wanakwenda kuiandika Tanzania kwenye vitabu vya historia ya soka la walemavu duniani.

Kinara wa mabao wa timu hiyo, Khalfan Kiyanga alisema watapambana sana.

“Akili zetu na nguvu zetu zipo katika kulitangaza soka la walemavu Tanzania kimataifa na kikubwa ni kuwa tunayo sapoti kutoka kwa Watanzania wenzetu kwani wanatuombea mema, alisena kuongeza:

“Lakini bado soka la walemavu halijapewa mkazo mkubwa hivyo wadau pamoja na serikali waongeze juhudi kuhakikisha wanatupa nguvu ya kusimama kwani tuna kiu ya kufanya makubwa zaidi kwa taifa letu.”

Naye nahodha wa Tembo Warriors, Juma Kidevu alisema timu hiyo imekuwa ikipambana uwanjani muda wote kwasababu wanajua Watanzania walionyuma yao wanahitaji ushindi hivyo wataendelea kufanya vizuri katika mashindano haya na yajayo.

Beki kisiki wa timu hiyo, Abdulkarim Khalfani alisema; “Walemavu tuna uwezo wa kufanya makubwa kama walivyo watu wengine hivyo hatuna sababu ya kuwa nyuma katika kuchangia maendeleo ya taifa letu katika sekta mbalimbali, kikubwa ni kujua kipaji chako na kukitumia kwa faida zaidi.”