Tanzania rasmi kuingiza timu nne CAF

Muktasari:

  • TFF wametoa taarifa rasmi ya Tanzania kuingiza timu nne katika mashindano ya kimataifa kwa msimu ujao.

SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini (TFF) limetoa taarifa rasmi ya Tanzania kuingiza timu nne katika mashindano ya kimataifa Afrika kwa msimu ujao baada ya kuwa miongoni  mwa nchi zilizokusanya alama nyingi zaidi kwenye viwango vya CAF.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 ambazo zitaingiza timu nne kwa msimu wa 2021/2022 , huku timu mbili zikiwa zinacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na timu mbili zingine zitacheza kombe la Shirikisho Afrika.

Hatua ya raundi ya awali itachezwa kati ya Septemba 10-12 na marudiano kati ya Septemba 17-19, 2021.

Upande wa hatua ya makundi katika mashindano hayoitachezwa kati ya Februari 11-13, 2022.

Tanzania upande wa timu ambazo zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni zile ambazo zitamaliza nafasi mbili za juu, huku upande wa Shirikisho Afrika ataenda Bingwa wa FA na mshindi wa tatu katika Ligi.

Mpaka sasa nafasi ya kwanza mpaka tatu katika Ligi Kuu inashikiliwa na Simba, Yanga na Azam huku upande wa Fa ikiwa hatua ya nusu fainali, zimeingia timu za Biashara Utd, Yanga, Azam na Simba.