Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars yaanza vibaya Chan

Timu ya taifa la Tanzania 'Taifa Stars' imeanza vibaya mashindano ya Chan nchini Cameroon baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Zambia 'Chipololo'.

Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza dakika ya 64 walilofungwa na  Collins Sikombe kwa mkwaju wa penalti baada ya Shomari Kapombe kushika mpira akiwa kwenye eneo la hatari akiwa katika harakati za kuzuia shambulio la Chipolopolo.

Tofauti na walivyocheza kipindi cha kwanza, Chipololo  walionekana kuwa bora zaidi ya Taifa Stars na kufanya mashambulizi ya nguvu na hatimaye wakapata bao la pili dakika ya 81 lililofungwa kwa maridadi na Emmanuel Chabula baada ya kufanyika makosa kwenye safu ya ulinzi ya kikosi cha Etienne Ndayiragije.

Kabla ya kufungwa bao la pili, Taifa Stars ilikuwa na nafasi nzuri ya kusawazisha bao la kwanza walilotanguliwa lakini Ditram  Nchimbi alipoteza nafasi ya wazi dakika ya 77 baada ya kupenyezewa pasi ya mwisho ya Farid Mussa.

Mshambuliaji huyo akitazamana na kipa wa Chipolopolo alipiga mpira kuudokoa ambao ulipaa juu ya lango la Allan Chibwe ambaye alionekana kuwa imara na kikwazo kwa Taifa Stars.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza Taifa Stars ilionekana kuutawala mchezo licha ya kuzidiwa idadi ya mashuti langoni  na wapinzani wao, Zambia.

Kwa dakika hizo za kipindi cha kwanza Taifa Stars ilikuwa na mashuti matatu lakini hapakuwa na hata moja lililolenga lango, Chipolopolo wao walikuwa na mashuti saba huku matatu kati ya hayo yakilenga lango ikiwemo lile la Emmanuel Chabula dakika dakika ya 29 ambalo lilichezwa na golikipa, Aishi Manula.

Miongoni mwa mashuti ya Tanzania ni lile lililopigwa na Feisal Salum dakika ya 21 baada ya kuanzwa kwa faulo ikutoka kwa winga ya kushoto na kuanzwa na  Edward Manyama ndipo mpira ule ulipomkuta kiungo huyo wa Yanga na kutandika shuti kali nje ya eneo la hatari lakini mpira ulipaa kwenye lango la Zambia.

Kuanzia dakika ya 25 hadi 27 Taifa Stars ilikuwa ikionyesha kuwa kusaka bao la kuongoza kwa kufanya mashambulizi mfululizo kupitia winga ya kulia ambayo alikuwa akicheza Yusufu Mhilu huku nyuma yake akisaidiwa kupandisha mashambulizi hayo na beki Shomary Kapombe.

Licha ya mshambulizi hayo mfululizo ilionekana kukosekana mshambuliaji wa kucheza krosi ambazo zilikuwa zikichongwa na wachezaji hao kutoka winga ya kulia.

Chipololo walionyesha kadi mbili za njano ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza baada ya kucheza mchezo ambao haukuonekana kuwa wakiungwana, kadi ya kwanza ilitolewa dakika 33 kwa Golden Mafwenta, akafuata Kelvin Mubanga Kampamba dakika ya tano baadaye.

Dakika ya 40, Ayubu Lyanga alipoteza nafasi ya kuitanguliza Taifa Stars baada ya kupigiwa pasi ndefu akiwa winga ya kushoto, aliingia vizuri kwenye eneo la hatari lakini alipiga shuti ambalo lilipaa juu ya lango la golikipa wa Zambia, Allan Chibwe.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko, walianza Zambia kwa kumtoa, Golden Mafwenta dakika ya 46  akaingia Spencer Sautu huku kwa Tanzania akitolewa Lucas Kikoti dakika ya 49 na kuingia Deus Kaseke.

Mabadiliko mengine kwa Taifa Stars ambayo yalifanyika kipindi cha pili walitoka Yusuf Mhilu na Ayubu  Lyanga huku wakiingia Farid Mussa na Adam Adam lakini hawakuonekana kuleta uhali kwa Taifa Stars na badala yake mabadiliko ya Zambia yaliyofanywa na kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojevic 'Micho' yalionekana kuwa na faida kwao.

Kwa kipigi hicho Taifa Stars inakuwa timu ya kwanza kufungwa mabao mengi (2) tangu yalipoanza Januari 16.

Mechi ijayo kwa Taifa Stars utakuwa Jumamosi dhidi ya Namibia na baada ya mchezo huo watatupa karata yao ya mwisho hatua ya makundi kwa kucheza, Jumatano ya Januari 27 dhidi ya Guinea.

Kikosi cha Zambia 'Chipolopolo' Allan Chibwe,Zacharia Chilongoshi, Golden Mafwenta, Luka Banda,Clement Mulashi,Kelvin Mubanga, Paul Katema, Kelvin Kapumbu, Spencer Sautu, Collins Sikombe na Emmanuel Chabula.

Kwa upande wa Taifa Stars kikosi kiliundwa na Aishi  Manula,Shomary Kapombe, Edward  Manyama,Bakari  Mwamnyeto,Kalos Protus,Baraka Majogoro,Yusufu  Mhilu, Feisal Salum 'Fei Toto', Ditram Nchimbi,Lucas  Kikoti na Ayubu  Lyanga.