Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga SC yajifungia na Sowah Dar

SOWAH Pict
SOWAH Pict

Muktasari:

  • Kuna asilimia zaidi ya 85 Sowah atakuwa Yanga msimu ujao baada ya kikao hicho cha siri kukamilika kwa mafanikio kutokana na mshambuliaji huyo kukubali kuwa, atasaini mkataba wa miaka miwili.

WAKATI Yanga ikianza maisha mapya bila kiungo mshambuliaji, Stephane Aziz KI anayedaiwa anajidaa kwenda Wydad Casablanca ya Morocco, mabosi wa klabu hiyo wamepiga hesabu kali za kuboresha kikosi hicho kwa msimu ujao na fasta wamekutana kwa siri na mshambuliaji Jonathan Sowah kisha kuweka sawa dili la Mghana huyo kusaini.

Kuna asilimia zaidi ya 85 Sowah atakuwa Yanga msimu ujao baada ya kikao hicho cha siri kukamilika kwa mafanikio kutokana na mshambuliaji huyo kukubali kuwa, atasaini mkataba wa miaka miwili.

Yanga imeweka sawa safari ya kumnasa Sowah ikiwa ni hesabu zao za kutaka kikosi chao kwa msimu ujao safu yao ya ushambuliaji iongozwe na Sowah na Dube.

Mabingwa hao tayari wanafahamu kwamba kuna nafasi kubwa ya kumuuza mshambuliaji Clement Mzize ambaye anagombewa na klabu za Ulaya na Afrika, huku ikiwa imeagana na Aziz KI aliyecheza mechi ya mwisho ya kikosi hicho wikiendi hii walipoitungua JKT Tanzania katika nusu fainali ya FA.

Inadaiwa kuwa, Yanga pia itaachana na mshambuliaji Kennedy Musonda mwisho wa msimu huu kufu-atia mkataba alionao kumalizika ambapo nafasi yake ya wachezaji wa kigeni itatumika kumuingiza Sowah anayekipiga kwa sasa Singida Black Stars akiwa amefunga mabao 11 kupitia mechi 11.

Ingawa Sowah bado ana mkataba na Singida BS lakini hatua hiyo haiizuii Yanga kumpata mshambuliaji huyo kutokana na kile ambacho staa huyo alikisema kwamba wakati Singida inamfuata kumsajili aliitaka itambue kwanza kwamba nyumbani kwake ni Yanga.

Sowah amefunga mabao 11 ndani Singida akiwa ameingia kupitia dirisha dogo la usajili Januari akionye-sha kasi kubwa ya kufumania nyavu.

“Ishu ya Sowah tumeshamaliza kila kitu, kilichosalia ni kusaini mkataba kamili wa kuitumikia Yanga, tun-ataka kuwa na safu bora yenye makali ya ushambuliaji kwa msimu ujao,” alisema bosi huyo wa juu.

“Tunataka Sowah aungane na Dube, ukiona namba za Dube kwenye msimu wake wa kwanza  Yanga zimetupa uhakika kwamba tulipata mtu sahihi licha ya kuanza kwa taratibu, lakini kama wawili hao wakicheza pamoja tutakuwa na safu bora zaidi ya ushambuliaji.”