Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga kwenye ligi ya hat trick

Muktasari:

  • Kwa misimu minne mfululizo kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi sasa nyota wa timu hizo ndio wanaoongoza kwa kufunga ‘hat-trick’, huku Simba ikiwa kinara baada ya kufunga nane, kwa upande wa wapinzani wao wakubwa, Yanga wakifunga sita.

LIGI Kuu Bara kwa msimu wa 2024-2025, inaenda ukingoni ambapo hadi sasa zimefungwa hat trick nne kutoka kwa wachezaji wa Simba na Yanga kila mmoja wao, ingawa nyota wa timu hizo wamekuwa ni moto wa kuotea mbali kwa wapinzani.

Kwa misimu minne mfululizo kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi sasa nyota wa timu hizo ndio wanaoongoza kwa kufunga ‘hat-trick’, huku Simba ikiwa kinara baada ya kufunga nane, kwa upande wa wapinzani wao wakubwa, Yanga wakifunga sita.

Katika misimu hiyo minne ni msimu mmoja tu wa 2021-2022 ambao zilifungwa ‘hat-trick’ tatu, huku wakikosekana wachezaji wa Simba na Yanga.

Katika msimu huo Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons, Shiza Kichuya (Namungo) na Idris Mbombo (Azam) walifunga hat trick kwenye mashindano hayo.

Msimu wa 2022-2023 zilifungwa ‘hat-trick’ tisa huku nyota wa Simba wakifunga tano ambapo aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho John Bocco alifunga mbili akianza na ya ushindi wa timu hiyo wa 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Novemba 19, 2022.

Bocco akafunga tena waliposhinda mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons Desemba 30, 2022, huku kiungo Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ akifunga pia mechi na Prisons kisha akatupia tena Simba ikishinda 6-1 mbele ya Polisi Tanzania, Juni 6, 2023.

Nyota mwingine wa tano aliyefunga ni Jean Baleke katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Machi 11, 2023, huku wa Yanga waliofunga ni Fiston Mayele wakati waliposhinda 4-1 mbele ya Singida Black Stars, Novemba 17, 2022.

Mwingine wa Yanga aliyefunga msimu huo ni kiungo mshambuliaji Stephane Aziz KI katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 5-0 dhidi ya Kagera Sugar, Aprili 11, 2023, ukiwa ni msimu uliotoa ‘hat-trick’ nyingi zaidi hadi sasa katika Ligi Kuu.

Msimu uliopita wa 2023-2024 zilifungwa ‘hat-trick’ saba, huku Simba ikifunga moja iliyokuwa ya nyota wa zamani wa timu hiyo Jean Baleke aliyoifunga katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 3-0, dhidi ya Coastal Union, Septemba 21, 2023.

Kwa upande wa Yanga walifunga ‘hat-trick’ mbili ambazo zote zilifungwa na kiungo Stephane Aziz KI akianza na ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam Oktoba 23, 2023, huku nyingine ni ile ilipoichapa Tanzania Prisons 4-1, Mei 28, 2024.

Msimu huu wa 2024-2025 timu zote zimefunga ‘hat-trick’ mbili ambapo kwa Yanga alianza Prince Dube katika ushindi wa 3-2, dhidi ya Mashujaa (Desemba 19, 2024) na ya Stephane Aziz KI aliyoifunga ilipoichapa KMC mabao 6-1, Februari 14, 2025. 

Kwa upande wa Simba, alianza mshambuliaji, Steven Mukwala katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, Machi 1, 2025, huku nyingine ni ya Jean Charles Ahoua wakati kikosi hicho kiliposhinda 5-1, mbele ya Pamba Jiji, Mei 8, 2025.

Kwa maana hiyo, tangu msimu wa 2021-2022 hadi sasa, wachezaji wa Simba ndio wanaoongoza kwa kufunga ‘hat-trick’ nyingi zaidi, baada ya kufanya hivyo mara nane, wakifuatiwa na nyota wa Yanga waliofunga sita huku Azam wakifunga nne.