Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu waongeza mzigo kwa Mzize, dili lipo hivi

Muktasari:

  • Mzize anayemiliki mabao 13 na asisti tatu katika Ligi Kuu Bara kwa sasa amekuwa kwenye rada za kkabu kadhaa zikiwamo za Ulaya, lakini inaelezwa kwa sasa mipango iliyopo ni kwamba muda wowote ataondoka Yanga kwa kuuzwa na klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa Aziz KI.

UKIONDOA jina la kiungo Stephanie Aziz KI aliyeuzwa Morocco, staa atakayefuata sasa ni straika Clement Mzize aliyebakiza wiki moja tu kuuzwa moja ya nchi ya Afrika Kaskazini baada ofa mbili kubwa kutua klabuni hapo kwa Waarabu kuongeza dau ili kumng’oa Yanga.

Mzize anayemiliki mabao 13 na asisti tatu katika Ligi Kuu Bara kwa sasa amekuwa kwenye rada za kkabu kadhaa zikiwamo za Ulaya, lakini inaelezwa kwa sasa mipango iliyopo ni kwamba muda wowote ataondoka Yanga kwa kuuzwa na klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa Aziz KI.

Ingawa mabosi wa Yanga wanafanya siri juu ya biashara hizo, lakini Mzize anahesabu siku tu kuuzwa baada ya klabu tatu za Wydad Athletic iliyomnunua Aziz KI, Zamalek ya Misri na Al Hilal Tripoli ya Libya zote zikifikia dau ambalo Yanga inalitaka.

Taarifa kutoka kwa wasimamizi wa mshambuliaji wa huyo ni kwamba klabu hizo tatu kila moja imekubali kutoa Dola 1 milioni (takriban Sh2.5 bilioni) kuwania saini ya Mzize na uongozi wa Yanga umeshawishika juu ya ofa hizo.

Inaelezwa Yanga imewashika Waarabu hao kufuatia mkataba wa mshambuliaji huyo aliobakisha, lakini kwa umri alionao na kiwango chake kwa sasa akiwa kwenye kasi ya kufunga mabao ni moja ya sababu ya klabu hizo kuongeza dau ili kunasa saini yake.

Msimu huu Mzize amekuwa na rekodi bora za kufunga mabao akifunga 13 akiwa mfungaji kinara namba mbili nyuma ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Jean Charles Ahoua mwenye 15 ambapo mshambuliaji huyo amelingana na mwenzake ndani ya Yanga, Prince Dube mwenye 13 pia.

Mbali na rekodi hizo pia Mzize bado ni mchezaji tegemeo wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambapo klabu yake imetumia nondo hizo kujiingizia fedha hizo ndefu.

Ingawa Mzize alikuwa mzito kukubali dili hizo za Afrika akitaka kwenda Ulaya, lakini inaelezwa vikao vya siri vinafanyika ili akubaliane na ofa moja kati ya hizo kabla ya kuruhisiwa kusafiri kwenda kumaliza dili hilo.

Bosi mmoja wa Yanga wa juu ameliambia Mwanaspoti kuwa Mzize ni mmoja wa mastaa ambaye kuna uhakika atauzwa msimu huu akitaka isubiriwe taarifa rasmi ya klabu ambayo itatolewa kwa ukamilifu wakati wowote wiki ijayo.

“Mzize yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao tutawauza. Kubaki kwa Mzize ni asilimia chache kuliko kuondoka, subirini uongozi utatoa taarifa kamili lakini kuuzwa ni lazima hiyo biashara ifanyike wakati wowote kutoka sasa,” alisema bosi huyo ndani ya Yanga.