Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara mpya wa Azizi Ki kufuru tupu

Muktasari:

  • Nyota huyo raia wa Burkina Faso, anakwenda kujiunga na Wydad baada ya kukitumikia kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa katika misimu mitatu, tangu Julai 15, 2022.

DILI la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI, kwenda Wydad Casablanca ya Morocco, limezidi kuutunisha mfuko wake kutokana na kile ambacho atakuwa akilipwa kwa mwezi.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso, anakwenda kujiunga na Wydad baada ya kukitumikia kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa katika misimu mitatu, tangu Julai 15, 2022.

Kitendo cha Aziz KI kukubali dili la kutua Wydad, amewekewa mshahara wa Dola 27,000 sawa na Sh72.3 milioni kwa mwezi ikiwa ni zaidi ya mara mbili aliyokuwa akilipwa ndani ya Yanga. Mshahara huyo unaweza kulipa wachezaji watatu wakubwa wa kigeni Jangwani na chenji ikabaki.

Taarifa zinabainisha kuwa, katika kikosi cha Yanga, kwa mwezi Aziz KI alikuwa akilipa Dola 13,000 sawa na Sh34.9 milioni ambao ndio ulikuwa mshahara mkubwa zaidi miongoni mwa mastaa wa kigeni.

Mkataba wa Aziz KI na Wydad anayoichezea Mtanzania Selemani Mwalimu 'Gomez', utakuwa wa miaka miwili akianza kucheza michuano ya Klabu Bingwa Dunia itakayofanyika Juni 15, 2025 hadi Julai 13, 2025, huko Marekani.

Wydad iliyopo Kundi G, itaanza michuano hiyo kwa kucheza dhidi ya Man City (Juni 18, 2025), kisha Juventus (Juni 22, 2025) na Al Ain (Juni 26, 2025.

Aziz Ki ameondoka Yanga akiacha rekodi ya aina yake baada ya kufunga jumla ya mabao 54 na asisti 32 katika mashindano yote, akicheza mechi 39 za Ligi Kuu huku msimu uliopita akishinda Tuzo ya Mfungaji Bora akifunga mabao 21.

Kwa misimu mitatu Aziz KI ametwaa makombe tisa akiwa na kikosi hicho yakiwemo mawili ya Ligi Kuu Bara, mengine mawili ya Kombe la Shirikisho (FA), Ngao ya Jamii mbili, Kombe la Muungano, Toyota na Mapinduzi yote akichukua moja kila shindano.

AZ 02

Mbali na mataji hayo, pia Aziz KI ameondoka nchini akiwa amebeba tuzo mbili za maana ikiwemo ya Mfungaji Bora na Mchezaji Bora wa msimu uliopita, hapo ni tofauti na za Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Bara zinazoendelea kutolewa.

Katika kipindi cha misimu yake mitatu, Aziz KI amefunga jumla ya 'Hat-Trick' tano ambapo nne kati ya hizo ni za Ligi Kuu Bara na moja michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), aliyoifunga msimu huu Yanga ilipoichapa Stand United mabao 8-1.