Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mbeya City anukia Mashujaa

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyewahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Coastal Union ya Tanga, Pamba Jiji ya Mwanza kisha kutua Mbeya City, amemaliza mkataba wa mwaka mmoja aliousaini huku kukiwa hakuna mazungumzo mapya ya kumuongezea mwingine wa kubaki.

VIONGOZI wa Mashujaa FC wako katika mazungumzo ya kupata saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Mudathir Said baada ya nyota huyo aliyeirejesha timu hiyo Ligi Kuu kumaliza mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho.

Nyota huyo aliyewahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Coastal Union ya Tanga, Pamba Jiji ya Mwanza kisha kutua Mbeya City, amemaliza mkataba wa mwaka mmoja aliousaini huku kukiwa hakuna mazungumzo mapya ya kumuongezea mwingine wa kubaki.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Mashujaa, Meja Abdul Tika alisema wameanza kufanya maboresho ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, ingawa kinachoendelea ni mazungumzo na wachezaji wanaowahitaji na wataweka wazi watakapokamilisha. 

“Kuna mapendekezo ya benchi la ufundi yaliyowasilishwa na sisi pia kama viongozi tumeanza kufanyia kazi mapema, hatuwezi kuweka wazi ni wachezaji gani ambao tunawahitaji kwa sasa kwa sababu za kiushindani zilizopo,” alisema Meja Abdul Tika.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Ally Nnunduma alisema tayari mipango ya kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao imeanza, ingawa ni mapema sana kuweka wazi ni mchezaji gani wanayemuhitaji au wale watakaoondoka.

“Suala la mchezaji kubaki au kuondoka tutaweka wazi tutakapokamilisha taratibu zote kwa sababu kuna mambo yanayoendelea ndani ya uongozi ambayo nisingependa kuyaeleza kwa sasa, jambo kubwa ni mashabiki zetu watarajie mazuri,” alisema Ally.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao mawili ya Ligi ya Championship msimu wa 2024-2025, akiwa na timu hiyo, inaelezwa ni pendekezo la Kocha wa Mashujaa, Salum Mayanga aliyemfundisha Mbeya City kabla ya kujiunga na kikosi hicho cha maafande.