Singida Big Stars yalamba dili na SportPesa
KLABU ya Singida Big Stars imeingia makubaliano ya miaka minne na kampuni ya kubashiri ya SportPesa.
Wageni hao wapya wa Ligi Kuu Bara wameingia mkataba huo ambao hata hivyo haujawekwa wazi juu ya kiasi cha fedha kilichowekwa.
Akizungumza na Mwanaspoti Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema sababu ya kutoweka wazi fedha za mkataba huo ni kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
"Tutakuja kutangaza fedha za udhamini huo huko baadae ila kwa sasa ifahamike tu hivyo kwamba mkataba ni wa miaka minne," alisema Ten aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa Muhibu Kanu ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Masoko na Fedha.