Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbu, Geay kukiwasha Mampando Festival

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Tamasha hilo litafanyika katika kijiji cha Mampando kilichopo wilayani Ikungi mkoani Singida lengo ikiwa ni kuibua na kuendelea vipaji vya vijana kupitia michezo.

Msimu wa nne wa tamasha la Mampando unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanza Juni 23, huku wanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Simbu na Gabriel Geay wakiwa miongoni mwa nyota ambao watakaokuwepo kulinogesha.

Tamasha hilo litafanyika katika kijiji cha Mampando kilichopo wilayani Ikungi mkoani Singida lengo ikiwa ni kuibua na kuendelea vipaji vya vijana kupitia michezo.

Simbu ambaye ni mratibu wa Mampando Sports Festival amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka, riadha, drafti, bao na kufukuza kuku.

Nyota huyo ameongeza kuwa tayari wanariadha wakubwa wa kimataifa wakiongozwa na Geay, Jackline Sakilu, Magdalena Shauri, Angela John, Faraja Lazaro na wengine wengi wamethibitisha kushiriki ili kuwa chachu ya hamasa kwa vijana wadogo ambao wanatamani kutimiza ndogo.

“Tangu ilipoanza kufanyika imetoa vipaji mbalimbali hasa kwa upande wa riadha kuna nyota ambao wametokea hapo na sasa hivi wanafanya vizuri kwenye mchezo huo,” amesema Simbu.

Nyota huyo amewataka wadau wa michezo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kushiriki na kuongeza kuwa wanatazamia mgeni rasmi siku ya kufunga Juni 25, mwaka huu kuwa Mkuu wa Wilaya Ikungi, Thomas Apson.