Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchujo kupita Singida Black Stars

MCHUJO Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka katika klabu hiyo iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, zinabainisha kikosi hicho kina wachezaji zaidi ya 10 waliotolewa kwa mkopo katika timu mbalimbali.

SINGIDA Black Stars ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, imepanga kufanya mchujo mkali kwa wachezaji iliowatoa kwa mkopo ili kufanya uamuzi wa kuendelea nao au kuwaacha.

Taarifa kutoka katika klabu hiyo iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, zinabainisha kikosi hicho kina wachezaji zaidi ya 10 waliotolewa kwa mkopo katika timu mbalimbali.

Bosi mmoja wa juu wa timu hiyo, ameliambia Mwanaspoti hadi sasa hakuna uhakika wa kundi hilo  kurudishwa, hivyo mchujo utakaofanyika utaamua.

Bosi huyo ameongeza katika kundi hilo, itafanyika tathimini ya viwango vyao kulingana na mikataba yao ilivyo na wale wasioridhisha wataondolewa moja kwa moja.

Alisema katika tathimini hiyo, pia wapo wachezaji ambao kama mikataba yao itakuwa mirefu, wataendelea kutolewa kwa mkopo kwenda kulinda viwango vyao na sio kuendelea kubaki hapo kukaa benchi.

“Tunawafuatilia hao wachezaji na hivi karibuni tumepokea ripoti ya hawa wote ambao wako kwa mkopo, mwisho wa msimu tutakaa na kuwafanyia tathimini.

“Wapo ambao tutaangalia namna ya kuachana nao kwa kuwa hatujaona mchango wao huko walipo. Kuna wengine tutaendelea kuwatoa kwa mkopo kwa kuwa mikataba yao ipo mirefu.

“Tunapata taarifa nyingi kwa uongozi wa klabu wanazozitumikia, kuna wengine tunapata taarifa zao za kinidhamu, haya yote yatatusaidia kufanya uamuzi,” alisema bosi huyo.

Mwanaspoti lilipomtafuta Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida Black Stars, Omary Kaya, alisema: “Tunasubiri ripoti ya mwisho ya kocha, mambo mengine tutayaamua baadae.”

Baadhi ya wachezaji ambao Singida Black Stars itawafanyia mchujo huo ni Benno Kakolanya, Raphael Daud Loth, Fikirini Bakari, Farhia Ondongo, Kelvin Sabato, Mukrimu Abdallah, Mohamed Camara, Habib Kyombo, Amadou Momade, Rabin Sanga, Benno Kakolanya na Zawadi Mauya.