Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kuanza na hawa usajili wa 2025/26

SITA Pict

MABOSI wa Simba katikati ya wiki walikutana kujadili mambo mbalimbali ikiwamo kupitia ripoti ya kocha Fadlu Davids ili kusuka kikosi cha msimu ujao huku wakiafikiana na pendekezo la kuanza na mashine sita.


Simba ilikuwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti Mohammed ‘MO’ Dewji sambamba na viongozi wa zamani ambacho pia kilifanya tathmini ya msimu uliomalizika na ripoti ya kocha inayohitaji usajili mzito.


Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimedokeza kuwa ukiacha tathmini ya msimu pia walijadili maandalizi ya msimu ujao na pendekezo la Fadlu anayetaka mashine mpya zisizopungua sita ili kuisuka Simba mpya itakayotetemesha ndani na nje ya nchi.

“Simba imefanya kikao hicho ambacho kitakuwa na mabadiliko katika baadhi ya maeneo ya kiuongozi na hata ya kikosi kwa ujumla,” kilisema chenzokutoka ndani ya Simba.

“Kubwa hasa ni kuhusu mahitaji ya kocha ambayo alipendekeza kama atasalia ndani ya kikosi na ni uhakika kuwa tutakuwa naye tena na hivyo mahitaji yake lazima yatimizwe.”

Kama ilivyoripitiwa jana ni kwamba, Fadlu pamoja na benchi la ufundi wamekubali kusaini mikataba mipya ya mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezwa mwingine baada ya kikao kizito kilichohusisha viongozi wa juu chini ya Mo Dewji.

Hatua hiyo imehitimisha sintofahamu iliyokuwapo juu ya hatma ya benchi la ufundi baada ya kushindwa kufikia mafanikio yaliyotarajiwa msimu uliopita, ambapo ilikuwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.


MASHINE SITA

Kwa mujibu wa chanzo hicho ni Fadlu amependekeza baadhi ya wachezaji wa kikosi cha sasa kuongezewa nguvu kwa kuletewa mashine sita ikiwamo eneo analocheza Jean Charles Ahoua aliyemaliza kinara wa mabao wa ligi akifunga 16 na asisti tisa.

“Ripoti ya awali ya Fadlu alihitaji Ahoua aongezewe nguvu zaidi. Pia anataka beki wa kati mwenye uwezo wa kukaba kwa akili na nguvu, kiungo mkabaji mwenye ubora kama au kushinda kagoma,” kilisema chanzo

“Kiungo mshambuliaji namba 10, mwenye ubora kushinda Ahoua, winga wa kulia mwenye makali kushinda Joshua Mutale na mshambuliaji wa kati mwenye ujuzi wa kufunga kushinda Mukwala (Steven) na Ateba (Leonel).”

Sababu kubwa ya kutaka mshambuliaji mwingine ni kutokana na taarifa kwamba huenda Mukwala anaweza kuchomoka baada ya kupata ofa yenye maana inayoweza kuipa timu hiyo fedha za maana kutoka klabu moja ya Afrika Kaskazini ambayo hata hivyo haijafahamika.

Hata hivyo, chanzo hicho hakijataja wachezaji waliopendekezwa moja kwa moja, lakini taarifa za mabosi wa klabu hiyo wameianza kazi ya kusaka beki mpya wa kati atakayetoka kati ya vikosi vya majeshi kama ilivyo kwa kipa atakayechukua nafasi iliyoachwa na Aisha Manula aliyerudi Azam FC. Klabu hiyo iliyofika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika na kulikosa taji mbele ya RS Berkane ya Morocco, inatarajiwa kuanza kambi ya maandalizi ya msimu ujao wiki mbili zijazo baada ya kumalizia mapumziko mafupi baada ya kumalizika msimu bila taji.

Simba ilimaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu nyuma ya Yanga iliyotetea taji kwa msimu wa nne mfululizo.