Simba hiyoo robo fainali Kombe la Shirikisho

Saturday May 01 2021
full pic 1
By Olipa Assa

SIMBA imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Kipindi cha pili Simba imeingi na plani ya kushambulia zaidi, jambo ambalo limewasaidia kupata mabao hayo.

Dakika ya 55 winga wa Simba, Benard Morrison aliibua shangwe za mashabiki wa timu hiyo, baada ya kusawazisha bao akipokea pasi ya Shomari Kapombe.

full pic 2

Bao hilo lilichangamsha safu ya ushambuliaji ya Simba kuanza kulishambulia langoni mwao  Kagera Sugar, baada kocha Didier Gomes, kufanya mabadiliko yakuwatoa Thadeo Lwanga/Morrison, Larry Bwalya/John Bocco.

Wakati Simba inashambulia, Kagera Sugar haikupoa, wachezaji wake walikuwa wanapambana kuokoa hatari na kufika langoni mwa wapinzani wao kwa kushitukiza.

Advertisement
half pic 2

Dakika ya 68 Simba imeendelea kucheka baada ya Meddie Kagere kufunga bao la pili na kuamsha mashabiki wao kuanza kupigwa nguma.

Dakika ya 84 Bocco amekosa bao la wazi baada ya kuwapiga chenga mabeki, kipa kisha kupiga pasi pembeni mwa goli.

half pic

Mabadiliko mengine kwa Simba, akitoka Meddie Kagere na kuingia Erasto Nyoni huku Kagera Sugar akiingia Seseme kuchukua nafasi ya Mwaijage.

Advertisement