Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba bab-kubwa

Mohammed ‘Shabalala’ akisaini mkataba wa kuichezea Simba, anayemuangalia ni Mwenyekiti wa Friends of Simba, Zacharia Hans Poppe.

Muktasari:

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Damas Ndumbaro, alisema wagombea wa Urais ni Andrew Tupa na Evans Aveva.

KAMPENI za uchaguzi Simba zimeanza jana Jumatatu mchana nchi nzima. Sambamba na hilo, bosi wa Friends of Simba ametangaza kuwa wameingia kazini rasmi na kusisitiza kwamba hatumwi mtoto sokoni.

Simba wameanza kwa fujo kwa kuwasajili, Mohammed Hussein Mohammed ‘Chabalala’, 19, beki wa kushoto wa Kagera Sugar na Ngorongoro Heroes.

Mwingine aliyemwaga wino jana na Chabalala ni Joram Nasson aliyetokea katika utaratibu wa kusaka vipaji uliofanywa na TFF. Wote hao wamesaini kuichezea Simba miaka mitatu.

Mwenyekiti wa Friends, Zacharia Hans Poppe ametamka kwamba Joram alikuwa njiani kwenda Yanga lakini wamemuwahi na sasa wanaleta mashine nyingine za maana zaidi kutoka Uganda, Kenya na Rwanda.

Aliongeza kwamba usajili huo unafuata kila sharti la kocha Zdravko Logarusic ambapo watasajili mshambuliaji wa kati, beki na kiungo mkabaji atakayewania namba na Jonas Mkude.

Alisema dhumuni la kumleta kiungo mkabaji ni kuwa na mbadala wa Mkude ambaye amekuwa akiipa shida timu hiyo mara anapoumia. “Huyo beki tumemalizana, sasa nawasiliana na wenzangu tukamilishe mchakato wa kuwaleta nyota watatu kutoka Uganda, Kenya na Rwanda,”alisema.

Aliongeza kwamba walishafanya mazungumzo na wachezaji na watakachofanya ni kuwachuja wachezaji wa kigeni kufikia watano.

Simba tayari ina wachezaji watano wa kigeni kipa Yaw Berko (amemaliza mkataba), Amissi Tambwe, Donald Mosoti, George Owino na Gilbert Kaze. Mwanaspoti lina uhakika kwamba Kaze na Berko wataachwa.

Aveva na Tupa wapitishwa

Kamati ya Uchaguzi ya Simba imetangaza orodha ya mwisho ya wagombea katika nafasi tatu za uchaguzi wa Jumapili ijayo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Damas Ndumbaro, alisema wagombea wa Urais ni Andrew Tupa na Evans Aveva.

Makamu Rais ni Geofrey Nyange, Swedi Mkwabi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Bundala Kabulwa huku wagombea ujumbe wakiwa 21 kati yao watatu wanawake.

Wagombea wanawake ni Amina Poyo, Asha Muhaji, Jasmine Badour wakati wanaume ni Said Tully, Ibrahim Masoud, Yasin Mwete, Ally Suru, Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo, Abdulhamid Mshangama, Chano Almasi, Damian Manembe, Kajuna Iddy, Hamis Mkoma, Alfred Elia, Said Kubenea, Maulid Abdallah, Collin Frisch, Idd Mkambala, Juma Mussa.

Wakati huohuo, wanachama watatu wa Simba kwa niaba ya wenzao 69 jana walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mchakato mzima wa uchaguzi huo.