Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sillah limebaki bao moja Ligi Kuu

Muktasari:

  • Sillah ambaye msimu uliopita alimaliza na mabao manane kwa  sasa anamiliki mabao tisa, alisema mechi za mwishoni zimekuwa ngumu, lakini akipata nafasi ya kucheza atapambana kadri awezavyo ili kufikisha idadi hiyo.

LIMEBAKIA bao moja ili itimie ndoto ya mshambuliaji wa Azam FC, Gibril Sillah anayetamani amalize msimu kwa mabao kuanzia 10, anaamini katika mechi mbili zilizosalia dhidi ya Tabora United na Fountain Gate linaweza likatokea hilo.

Sillah ambaye msimu uliopita alimaliza na mabao manane kwa  sasa anamiliki mabao tisa, alisema mechi za mwishoni zimekuwa ngumu, lakini akipata nafasi ya kucheza atapambana kadri awezavyo ili kufikisha idadi hiyo.

“Unaweza ukaona limebakia bao moja ni kitu rahisi, ukweli ni kwamba mechi zilizosalia na timu tunazokutana nazo zinapambania nafasi katika msimamo wa Ligi Kuu, hivyo tunahitaji kuongeza nguvu zaidi ya mapambano,” alisema Sillah na kuongeza;

“Ingawa jambo la msingi ni timu  kupata matokeo mazuri kwa maana nikiona mchezaji mwenzangu yupo eneo la kufunga nikiwa na mpira mguuni nitampa pasi yeye na siyo kujiangalia binafsi.”

Kilichomfurahisha zaidi msimu huu ni ushindani wa ligi uliyochangia wachezaji kucheza kwa viwango vya juu, vilivyoleta ugumu wa kutopata matokeo kirahisi kwa mechi za nyumbani na ugenini.

“Ligi ya Tanzania ni bora, kila unapopata nafasi ya kucheza lazima ujitathimini jinsi ya kuboresha kiwango kitakachokusaidia kulinda nafasi anayopata kikosi cha kwanza,” alisema.