Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti, Cameroon wanatua na ndege moja

Muktasari:

Wakati huo huo, Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amethibitisha kuwa straika wake, Kelvin John anaendelea vizuri. Straika huyo huyo anayetambulika kwa jila la utani la Mbappe aliumia kwenye michezo kule Rwanda katika mchezo dhidi ya Cameroon.

TIMU za vijana chini ya miaka 17, Tanzania na Cameroon zinatarajia kuingia nchini alfajiri ya leo Jumatatu saa tisa na dakika 40 (3:40) na ndege ya Ethiopia Airlines zikitokea Rwanda.

Timu hizo zilikuwa Rwanda katika mashindano ya kirafiki yaliyoandaliwa na kuzikutanisha timu tatu, Rwanda (wenyeji), Tanzania na Cameroon.

Kikosi cha Cameroon kinatarajia kuingia alfajiri ya leo huku kikitarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki nchini kabla ya fainali hizo kuanza Jumapili hii.

Pia, mabingwa wa mashindano hayo ya Rwanda, Serengeti Boys nao wanatua muda huo kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kuanza kuonyesha cheche zao kwenye Afcon.

Wakati huo huo, Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amethibitisha kuwa straika wake, Kelvin John anaendelea vizuri. Straika huyo huyo anayetambulika kwa jila la utani la Mbappe aliumia kwenye michezo kule Rwanda katika mchezo dhidi ya Cameroon.

“Kelvin John alipata majerahalakini kwa sasa anaendelea vizuri,” alisema Mirambo.