Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra gumzo Yanga ikikagua uwanja, Simba yakausha

DIARRA Pict

Muktasari:

  • Wakati wachezaji wenzake wakiwa ndani ya uwanja, yeye alikuwa anazunguka nje ya eneo la kuchezea na kuchezea nyavu za goli la upande wa kaskazini wanapokaa mashabiki wa Simba.

KIPA namba moja wa Yanga, Djigui Diarra ameibua gumzo muda mchache baada ya kikosi hicho kuingia kukagua Uwanja wa Benjamini Mkapa ambao unatarajiwa kupigwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba.

Wakati wachezaji wenzake wakiwa ndani ya uwanja, yeye alikuwa anazunguka nje ya eneo la kuchezea na kuchezea nyavu za goli la upande wa kaskazini wanapokaa mashabiki wa Simba.

Wachezaji wa Yanga wote waliingia sehemu ya kuchezea isipokuwa Diarra ambaye aliishia kuzunguka eneo dogo la uwanja upande wa mashabiki wa Simba, kisha akarejea vyumbani.

Wakati nyota wa Yanga wakifanya hivyo, kwa upande wa Simba hawajafanya zoezi hilo na kumuacha kocha wa viungo kuingia sehemu ya kuchezea na kuamsha amsha mashabiki.

Wakati huohuo, licha ya timu ya Yanga kuingia uwanjani kukagua uwanja, mashabiki wa timu hiyo hawakuwa na shangwe kama ilivyozoeleka timu hizo zinapoingia uwanjani.