Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Simba, Yanga wataka mageti yafungwe

MAGETI Pict

Muktasari:

  • Wakati Simba ikiingia tu, mashabiki wa Yanga wakashangilia kwa nguvu, kisha wakaanza kuwapigia kelele askari wa getini wakiwataka kufunga geti.

MASHABIKI wa Yanga wakorofi sana, hebu soma hii. Wakati Simba ikimaliza kuingia geti kubwa la Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuna kituko watani wao wakakifanya hata polisi imebidi wacheke.

Wakati Simba ikiingia tu, mashabiki wa Yanga wakashangilia kwa nguvu, kisha wakaanza kuwapigia kelele askari wa getini wakiwataka kufunga geti.

Mashabiki hao wametoa kauli hiyo wakisema hawataki kufanya makosa tena kuona Simba inakimbia uwanjani.

Shabiki mmoja wa Yanga, Said Hamsini, amesema wameisubiri mechi hiyo tangu Machi 8, 2025, ambapo iliahirishwa baada ya Simba kutoa tamko la kutocheza kisha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ikatangaza rasmi.

"Hawa tumewasubiri sana, angalia kuanzia Machi 8 wamekimbia walifika mpaka hapa Machi 7 lakini hawakutokea siku ya mchezo," amesema Hamsini.

"Pale tulikuwa tunawaomba polisi wafunge geti wasije wakaleta kipengele kingine wakakimbia, leo tunataka tumalizane nao."

Kauli ya shabiki huyo wa Yanga na wenzake ikawafanya askari wa getini kucheka wakishtukia kwamba jamaa wanaendeleza utani wao.