Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yaivaa Rwanda leo, majeruhi Kelvin ‘Mbappe’ hatihati kucheza Afcon Dar es Salaam

Muktasari:

 

  • Kelvin anatarajia kuukosa mchezo wa mwisho wa kirafiki kujiandaa na Afcon dhidi ya wenyeji Rwanda kutokana na kupata majeraha katika mchezo wa kwanza na Cameroon.

Dar es Salaam. Mshambuliaji nyota wa Serengeti Boys, Kelvin John ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Rwanda kutokana na kuuguza majeruhi mguu aliyopata katika mchezo dhidi ya Cameroon.

Taarifa kutoka Rwanda zinadai mshambuliaji tegemeo wa Serengeti Boys ameumia nyama za paja ambazo zinaweza kumkosesha kucheza fainali za Afcon zitakazofanyika Dar es Salaam kuanzia Aprili 14-28.

Kutokana na majeruhi hayo Kelvin ‘Mbappe’ imewapa kigugumizi benchi la ufundi la Serengeti Boys kuzungumza hatma ya nyota huyo.

Chanzo cha ndani kutoka ndani ya kambi hiyo kimeweka wazi kuwa ni kweli anaendelea vizuri, lakini bado ajaanza mazoezi kutokana na tatizo hilo na yupo chini ya uangalizi maalumu.

"Kelvin alipata tatizo kubwa tofauti na inavyoripotiwa alichanika nyama za paja anaendelea vizuri yupo chini ya uangalizi wa daktari kuhusiana na mazoezi bado hajaanza sijajua ataanza lini, lakini timu inatarajia kurudi Dar es Salaam Aprili 6 mwaka huu," kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilimtafuta daktari wa Serengeti Boys, Joakim Mshanga kulizungumzie suala la Kelvin alisema anaendelea vizuri kesho anaweza kuanza mazoezi na kuweka wazi kuwa yeye sio msemaji wa hilo hivyo hawezi kuzungumzia kiundani.

"Naomba nikutumie namba ya Daktari Emil Urassa anaweza akakupa maelezo mazuri mimi sio daktari ni physiotherapist hivyo siwezi kulizungumzia suala hilo kiundani, lakini kwa taarifa nilizonazo Mbappe anaweza akaanza mazoezi kesho," alisema Mshanga.

Hata hivyo namba ya Daktari Urassa ilipopigwa jana Jumatano saa 8:15 mchana, na kurudiwa tena saa 9:30, alasiri haikupatikana hata leo Alhamisi asubuhi saa 3:47 bado siku hiyo haikupatikana.

Alipotafutwa Kocha wa Mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema hawawezi kuhatarisha afya ya Kelvin kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Rwanda leo.

Mirambo alisema amesafiri na nyota wengi kwaajili ya kujiandaa na mashindano yaliyombele yao hivyo kuumia kwa Kelvin ambaye kwa sasa anaendelea vizuri hawawezi kulazimisha acheze dhidi ya Rwanda wanampumzisha kwaajili ya mashindano.

"Alipata maumivu kidogo, lakini kwa sasa anaendelea vizuri japo nimeamua kumpumzisha na nafasi yake itachukuliwa na nyota wengine tuliosafiri nao ukizingatia Rwanda ni timu ambayo tumecheza naye mara nyingi na tumepata matokeo," alisema Mirambo.

Baada ya mchezo dhidi ya Cameroon walioshinda 2-1, Mirambo alisema Kelvin yupo fiti licha ya kutoka nje na kushindwa kuendelea na mchezo huo.

“Anaendelea vizuri aliangaliwa na madaktari kwa ukaribu na ikaonekana ni misuli tu ndio ilimfanya ashindwe kuendelea na mchezo baada ya kukanyagwa, alipatiwa matibabu madogo ya kuondoa maumivu na hivi sasa yuko sawa,” alisema Mirambo.