Rashid Juma, Kaheza wawapisha Maguli na Maganga

Friday November 19 2021
Ruvu KIKOSI PIC
By Damian Masyenene

Kocha Msaidizi wa Ruvu Shooting, Mohamed Nakuchema ameanza na Elias Maguli na Fully Zulu Maganga katika Safu ya ushambuliaji kuikabili Simba katika mchezo wa Ligi Kuu leo Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Nyota hao wanachukua nafasi za Rashid Juma na Marcel Kaheza walioanza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga waliolala kwa mabao 3-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Maganga amekabidhiwa majukumu ya nahodha wa kikosi hicho katika mchezo wa leo.

Beki Cassin Ponera ameanza akichukua nafasi ya Santos Mazengo aliyeonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.

Kikosi cha Ruvu Shooting hakijabadilika sana kwani ni nyota hao watatu pekee ndiyo hawakuanza katika mchezo uliopita.

Kikosi cha Ruvu Shooting kitakachoanza ni Mohamed Makaka, Nathaniel Chilambo, Paul Ngalema, Cassian Ponera, Michael Masinda, Zuberi Dabi, Ally Kombo, Pius Buswita, Elias Maguli, Fully Maganga na Shaban Msala.

Advertisement

Wachezaji wa akiba ni Bidii Hussein, Eradius Mfulebe, Renatus Ambrosi, William Patrick, Marcel Kaheza, Abrahman Mussa, Sadat Mohamed na Said Zanda.

Advertisement