Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia kuneeemesha wanamichezo

Rais Samia kuneeemesha wanamichezo

Dodoma. RAIS Samia Suluhu Hassan amesema wasanii na wanamichezo wana fursa kubwa ya kukua na Serikali imeendelea kuwapa nguvu kwa kuwatungia sera nzuri na sheria.
Rais Samia aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipofanya mahojiano maalumu ya kutumiza mwaka mmoja madarakani tangu aapishwe kushika wadhifa huo, Machi 19, 2021 baada ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.
Mahojiano hayo yalifanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na Kampuni ya Mwananchi Communications ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na Mwananchi Digital yaliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bakari Machumu.

Rais Samia alisema hayo baada ya kuulizwa swali kuhusiana na mkakati wa Serikali wa kuwaendeleza vijana na wanamichezo nchini.

Alisema vijana kwenye sekta zote ikiwamo michezo Serikali itawajengea uwezo wahusika ili wajitegemee.
“Wana fursa kubwa ambayo na sisi tunawapa nguvu tunatoa sera nzuri, tunawatungia sheria nzuri ili waweze kukua. Tumeanza kulipa mirahaba kwa hawa wasanii, wenye nyimbo zao, wenye michezo yao. Tumeanza kuwalipa ili wakue waweze kujikuza, kampuni zao zikue ili waende kimataifa,” alisema Rais Samia.

Alisema lengo la Serikali ni kuwafanya wawe na nguvu kazi ambayo inaweza ikazalishwa nchini.
Rais Samia pia Serikali inataka kuwajengea uwezo ambao utawawezesha kufanya biashara zao, wakajenga mashirika yao, wakaweza kujitegemea, wakawa Watanzania ambao wanaweza wakaendesha maisha.
“Lakini, wakaweza kuiuza nchi yao nje hasa hao uliowataja wa michezo na sanaa. Wakaweze kuuza vizuri nchi yao nje,” alisema.
Rais Samia alitoa mfano wa namna muziki wa singeli ulivyovuta watu kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dubai Expo2020 kwamba, mwanamuziki wa muziki wa huo kutoka Tanzania alijaza watu kwenye banda la Tanzania.

“Tulikwenda na vijana wa utamaduni vikundi vitatu, sijui vinne vile, lakini wameonyesha, wameuza nchi yao.
“Siku ile Tanzania tulijaza kuliko nchi zozote zile mpaka watu wanauliza leo nchi gani mbona pamejaa kwa sababu yule wa singeli yeyeeee, yeeee, yeeee sijui nini. Watu hawajawahi kuona hiyo.
“Lakini (watu) wamekuja tele wamekuja kuangalia pale, tulikuwa na kikundi cha taarabu, mtu kavaa baibui yake na kanga yake kiutamaduni anaimba vizuri, watu wamejaa,” alisema Rais Samia.
Alisema inachofanya Serikali ni kuweka mazingira mazuri na kwamba sera na mipango ipo kwa ajili ya vijana wote wa Kitanzania.