Prisons: Azam washukuru kwa sare hii

Tuesday February 23 2021
prison pic
By Thomas Ng'itu

KOCHA msaidizi wa klabu ya Prisons, Shaban Kazumba amesema Azam washukuru kupata pointi moja katika mchezo wao kwani wao walikuwa wanataka kupata pointi tatu.

Kazumba alisema wakiwa wanaenda kucheza mchezo huyo lengo lilikuwa ni kuibuka na ushindi lakini kwa sare hiyo wanaipongeza Azam FC.

"Kupata pointi moja katika uwanja wao wa nyumbani sio kitu kibaya kwao na hata kwetu pia, pointi hii itatusaidia kututoa sehemu moja kwenda nyingine".

Kazumba alisema ameshukuru wachezaji wake muda wote walikuwa makini kufata maelekezo ambayo walikuwa wakiwapa muda wote wa mchezo.

prison pic 1

"Tulikubaliana tunashambulia wote na kukaba wote na  hilo ndilo lililofanyika, kama ingetokea tungekata mapema basi Azam wangepata ushindi".

Advertisement

Azam na Prison zilitoka sare tasa mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Chamazi Complex.

Advertisement