Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Owino asajili beki wa kati Msimbazi

Owino

Muktasari:

Simba ilikubali masharti na ikaanza kwa kumsajili Mrundi Gilbert Kaze aliyeletwa kwa ushawishi wa Amissi Tambwe na baadaye ikamleta Mkenya Donald Mosoti. Lakini sasa hivi Owino amebadilika na kudai kuwa Simba haihitaji kwenda tena nje ya nchi kusajili mabeki wa kati au pembeni, iangalie mabeki wa hapa hapa nchini.

BEKI wa Simba, Joseph Owino aliposajiliwa Simba mwaka jana alitaka viongozi wasajili beki mwingine wa kati ambaye ni raia wa kigeni kwasababu kwa wakati huo aliona Tanzania wapo wachache .

Simba ilikubali masharti na ikaanza kwa kumsajili Mrundi Gilbert Kaze aliyeletwa kwa ushawishi wa Amissi Tambwe na baadaye ikamleta Mkenya Donald Mosoti. Lakini sasa hivi Owino amebadilika na kudai kuwa Simba haihitaji kwenda tena nje ya nchi kusajili mabeki wa kati au pembeni, iangalie mabeki wa hapa hapa nchini.

Owino alisema,” Kuna mabeki wazuri kama yule wa Tanzania Prisons (Nurdin Chona) ambaye ana nguvu sana lakini Simba inahitaji kumchukua beki wa Ashanti United (Mohamed Faki )ambaye alikuwa alimkaba Tambwe mwanzo mwisho kwenye mchezo wa Simba na Ashanti ambao Simba tulipoteza 1-0.”

Owino alisema, “ Simba isitoke tena nje ya nchi kutafuta beki, yule wa Ashanti aliyemkaba Tambwe kiukweli ni mzuri sana kwani anakaba kwa akili, hachezi rafu na ana uwezo wa kuichezea Simba.”

“Kuna beki wa Prisons (Chona) ambaye pia anajua kudhibiti vizuri, sema anacheza rafu ya kawaida lakini ni beki mahiri sana na ana uwezo mkubwa,” alisema Owino ambaye anafikiria kwenda Iceland kucheza soka la kulipwa.

Beki wa Ashanti, Mohamed Faki alisema, “ Nimemaliza mkataba na Ashanti, kwasasa niko huru nikingoja kuzungumza na timu yoyote itakayonihitaji kimsingi naangalia wapi nitakapopata maslahi mazuri hivyo Simba waje tuzungumze.”

Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema: “Kila kitu cha usajili wa Simba kitawekwa wazi katikati ya wiki hii, hivyo ni mapema kusema lolote juu ya hilo.”