Nyota Madola ageukia muziki

Mwanariadha nyota wa zamani na mshindi wa medali ya fedha ya marathoni kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1998, Saimon Mrashani ameibukia kwenye muziki wa injili.
Mrashani ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu ya riadha ya Polisi, leo ametambulisha moja ya nyimbo zake katika tamasha la Karatu linaloendelea kwenye uwanja wa Mazingira bora mjini Karatu.
Katika tamasha hilo lililodhaminiwa na Olympic Solidarity (OS) kupitia kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Mrashani ameimba wimbo wake mpya wa Upendo akishirikiana na kikundi cha kwaya cha Muungano.
"Nilianza kuimba mwaka juzi (2019) miaka kadhaa baada ya kustaafu na ni muimbaji kwaya kwenye kanisa langu uko Tarime," anasema Mrashani ambaye pia amewahi kushinda medali ya shaba ya michezo ya Afrika ya 1995 nchini Zimbabwe.