Nyoni: Ahsanteni mashabiki

Thursday June 23 2022
nyoni pic
By Clezencia Tryphone

EKI wa Simba, Erasto Nyoni amewashukuru mashabiki wao kwa namna walivyowapa sapoti licha ya kwamba wameshindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu huu.

Yanga tayari wametangazwa mabingwa wapya wa ligi hiyo huku wakisubiri pia kucheza mechi ya fainali ya ASFC dhidi ya Coastal Union inayotarajiwa kuchezwa Julai 2, mwaka huu jijini Arusha.

Simba msimu huu umekuwa mbaya kwao kutokana na kupoteza makombe yote muhimu la Ngao ya Jamii, Ligi Kuu sambamba na la ASFC.

Nyoni alisema, juhudi ambazo wachezaji uzifanya katika timu mashabiki wanachangia kwa hali kubwa chachu ya mafanikio ya timu yao na msimu huu wameanguka wote. “Mashabiki wetu ni watu muhimu sana na wa kipekee, tulianza pamoja tunamaliza pamoja ni jambo la kujivunia sana, kupoteza makombe kila mwanasimba kaumia lakini ndio mpira,” alisema Nyoni.

Alisema wanajitahidi michezo iliyobaki wapate matokeo mazuri licha ya kushindwa kuchukua taji hilo mara tano mfululizo.

Simba imebakiza kucheza na Mtibwa Sugar (Mkapa), Prisons (Sokoine) na Mbeya Kwanza (Majimaji).

Advertisement
Advertisement