Ni neema kwa wanasoka

Tuesday September 14 2021
neema pic

Dar es Salaam. Katika kuongeza thamani kwenye michezo ya kubahatisha, kampuni ya Betway imezindua kituo cha kisasa cha kushuhudia michezo na kubashiri kistaarabu ‘Betway Sports Experience Center.’

Kituo hicho ni sehemu itakayowakutanisha wapenzi wa michezo kushuhudia michezo mbalimbali na kufanya ubashiri katika mazingira ya kuvutia.  Pia kituo cha elimu kuhusu michezo na namna ya kubashiri kistaarabu.

"Tuna furaha kubwa kuzindua kituo hiki cha kipekee na muhimu kwa mashabiki wa michezo nchini Tanzania kuweza kukutana na kufurahia kwa pamoja na kwenye mazingira ya kuvuti,” alisema  Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo Jimmy Kennedy.

Aliongeza “Hii ni sehemu ya ahadi yetu kuongeza thamani katika michezo ya kubashiri na sekta ya michezo kwa ujumla kwa sababu kituo hiki kitakuwa kama kitovu cha michezo ambapo mashabiki wataweza kukutana, kutazama michezo, na kufanya ubashiri wao kwa njia bora ambayo haijawahi kutokea hapo awali," alisema wakatiu wa uzinduzi.

Kwa upande wake, Michael Valentine, aliyejitambulisha kuwa ni shabiki wa timu ya Manchester United alikuwa ni moja ya waliohudhuria katika hafla hii na kueleza kuwa alijionea utofauti mkubwa katika kituo hicho cha Betway.


Advertisement
Advertisement