Nabi: Ni Makambo na Mayele

Wednesday November 17 2021
NABI PIC
By Thobias Sebastian

KOCHA wa Yanga, Nesreddine Nabi amesema kikubwa ambacho amekifanya wakati huu ni kutengeneza ubora wa wachezaji wake wake ambao hawapo katika kikosi cha kwanza kulingana na wanaocheza mara kwa mara.

Nabi alisema hataki kuona utofauti mkubwa uliopo kwa Heritier Makambo na Fiston Mayele au Kibwana Shomary dhidi ya David Bryson wote wanatakiwa kulingana ubora na kufanya kazi kubwa muda wote.

Alisema ili ikitokea mmoja amekosekana kama ambavyo ilikuwa katika mechi iliyopita hakuwepo, Khalid Aucho na nafasi hiyo alicheza Mukoko Tonombe ambaye alikuwa katika kiwango bora na kufunga.

“Naimani kubwa mno na wachezaji wangu wote waliobaki katika timu wakati huu na wale waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa wakikutana watakuwa wote katika hali ya ushindani,” alisema Nabi na kuongeza;

“Baada ya kukutana kwa pamoja tutafanya tathimini ya wote na kuona wachezaji ambao wanastahili kupata nafasi ya kucheza katika mechi hiyo ya Namungo ambayo natambua itakuwa ngumu,”

“Tunawafamu Namungo wanatimu nzuri, tumewaona wakicheza na Simba walionyesha kiwango bora kwahiyo wakati huu tunaendelea na kufanya maandalizi ya hali ya juu ili kuvuna pointi tatu kama ambavyo ilikuwa kwenye mechi tano za ligi zilizopita.” Yanga mpaka sasa inaongoza msimamo wa Ligi.

Advertisement
Advertisement