Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa bondia Ibrahim Najim kuzikwa Kyela

Marehemu,Najim Mohammed (kulia) akipambana na Laurent Segu Jumapili katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.Baada ya pambano hilo alikimbiza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) hadi jana mauti yalipomkuta.

Muktasari:

  • Najum alianguka ulingoni jumapili iliyopita baada tu ya kumalizika kwa pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia  Laurent Segu wa Dodoma  na kuwahishwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General).

Dodoma.Mwili wa  bondia wa ngumi za kulipwa nchini,  Ibrahim Najim unatarajiwa kuzikwa wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Najum alianguka ulingoni jumapili iliyopita baada  ya kumalizika kwa pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia  Laurent Segu wa Dodoma  na kuwahishwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General).

Katika pambano hilo, Najim alipigwa kwa pointi na inadaiwa  alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi asubuhi ya jana  hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na mauti mchana wa jana

Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu  ya ngumi za kulipwa pamoja na la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda moja na kupoteza mawili.

Kaka wa marehemu Richard Chawinga amesema wapo njiani wakielekea Kyela kwa ajili ya mazishi ya mabondia huyo na wakifika watakaa kikao kujua anazikwa lini.

“Tupo njiani tukielekea Mbeya tukifika ndio tutajua utaratibu wa mazishi upoje maana kuna ndugu zetu wanatusubiria kule, ila tutamhifadhi nyumbani Kyela”amesema Chawinga.