Mwadui watua kimya kimya Kambarage

Muktasari:
Baada ya Simba kuwasili uwanjani huku wakipokelewa kwa shangwe na mashabiki wake, Mwadui wao wameingia kimya kimya.
Shinyanga. Baada ya Simba kuwasili uwanjani huku wakipokelewa kwa shangwe na mashabiki wake, Mwadui wao wameingia kimya kimya.
Licha ya timu hiyo kuwa mwenyeji wa mechi hiyo, lakini haikuonesha dalili zozote kama wapo nyumbani.

Kikosi hicho kimetua saa 2:46 mchana na kwenda moja kwa moja vyumba vya kubadilishia nguo tayari kwa kuwavaa wapinzani hao.
Mashabiki wa Simba ambao wamejazana kwenye jukwaa zilipofikia timu, Mwadui iliambulia kelele na zomeazomea kutoka kwa wanazi hao wa Wekundu.