Mapema tu mashabiki wafurika Kambarage

Muktasari:
Mashabiki wamefurika uwanjani Kambarage wakiiwahi mechi ya Mwadui na Simba inayotarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni.
Shinyanga. Dakika chache baada ya kufunguliwa milango kwa ajili ya kuzama uwanjani kusubiri mpambano wa Ligi Kuu kati ya Mwadui na Simba, mashabiki wamefurika huku makomandoo wakifanya kazi ya ziada kuwaweka katika mpangilio maalumu.

Milango imefunguliwa majira ya saa 6:00 mchana huku foleni ikiwa tayari imeshafurika kwa mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ambapo jezi za Simba ndio zimetawala viunga hivyo vya CCM Kambarage.

Hadi sasa hali ya usalama imetanda ambapo licha ya mashabiki kuwa wengi nje ya uwanja, lakini wameoesha kufuata utaratibu kwa kuoanga msitali wenye konakona zaidi ya saba.

Mmoja wa makomandoo ambaye hakutka kutajwa majina yake amesema licha ya mashabiki kujitokeza kwa wingi lakini wanafuata maelekezo.
"Hatutumii nguvu nyingi, tunashukuru watu wamekuwa wastaarabu unaona walivyopanga foleni hakuna cha mtoto wala mkubwa, tunataka mtu afurahie kile kilichomleta" amesema Komandoo huyo.