Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa, Polisi kuamua krismasi leo

LEO kwenye Uwanja wa Gairo Morogoro, Mtibwa Sugar na Polisi Tanzania zitakuwa zikichuana kutafuta matokeo ambayo yatazifanya kula sikukuu ya Krismasi bila mawazo.

Hiyo ni kutokana na pointi za timu hizo mbili na nafasi zilipo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambapo Polisi ipo nafasi ya nne na alama 15 ikihitaji ushindi ili kufikisha pointi 18 na kula Krismasi ikiwa nafasi ya tatu.

Hivyo hivyo, Mtibwa iliyoko mkiani na alama sita, itaingia uwanjani kutafuta ushindi ambao utaifanya ifikishe pointi tisa na kupanda hadi nafasi ya 11 na kula Krismasi bila ‘stresi’ za kushuka daraja.

Hayo yote yataamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika na makocha wa timu zote mbili wameeleza kujipanga kuondoka na ushindi.

Kocha msaidizi wa Mtibwa, Awadh Maniche alisema wameandaa vizuri kikosi wakitarajia ushindi.

“Tunatambua ubora wa wapinzani wetu, tumeandaa vizuri kikosi na tupo tayari kwenda uwanjani kutafuta ushindi muhimu kesho (leo),” alisema Maniche.

Naye Malale Hamsini wa Polisi alisema kuwa timu ipo Morogoro tangu juzi na hiyo ni katika kuonyesha ni namna gani wamejipanga kushinda mechi hiyo.

“Tulifika Morogoro mapema baada ya mechi na Dodoma Jiji, tumefanya mazoezi mepesi na sasa tupo tayari kuwakabili Mtibwa,” alisema Malale.

Michezo miwili iliyopita ya ligi Mtibwa ilishinda moja dhidi ya Biashara (2-0) na kutoa suluhu dhidi ya KMC, huku Polisi ikishinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na sare 1-1, dhidi ya Dodoma Jiji.