Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moloko, Mayele, Fei wabaki Dar Yanga ikitua Zanzibar

Moloko, Mayele, Fei wabaki Dar Yanga ikitua Zanzibar

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Yanga wamewasili kisiwani Unguja tayari kwa mechi yao ya kesho Jumatano dhidi ya Taifa Jang'ombe huku nyota wao watano wakibaki jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao wamewasili Zanzibar bila nyota wao Jesus Moloko, Fistob Mayele, Farid Mussa, Dickson Job, Feisal Salum na kocha msaidizi Cedrick Kaze naye hakuwa miongoni mwa kikosi hicho.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema Kaze alienda kwao Burundi lakini tayari amewasili jijini Dar es Salaam na anatarajia kujiunga nao leo usiku ingawa wachezaji hao wataingia kesho Jumatano.

Hafidh amesema kuwa; "Waliobaki Dar ni wale waliokuwa wamepewa ruhusa ya mapumziko lakini kesho watakuja hivyo kikosi kitakuwa kimekamilika, upande wa Kaze alikuwa na matatizo ya kifamilia ila tayari amerejea na anakuja leo usiku.

"Tumekuja kutetea kombe letu. Tumelileta na tutarudi nalo, wachezaji wapo vizuri naamini tutafanya vyema," amesema Hafidh