Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahoua, Mpanzu wapewa kazi maalum Simba

KAZI Pict

KIKOSI cha Simba kinaendelea na maandalizi ya mwisho ya kuvaana na Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu ya kutimiza raundi ya 30, kisha kujipanga kwa pambano la Dabi ya Kariakoo, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids akiwageukia nyota wa kikosi hicho na kuwapa kazi maalumu.


Fadlu anayetua Msimbazi msimu huu akitokea Raja Casablanca ya Morocco alikokuwa kocha msaidizi na ameifanya timu hiyo kuwa tishio ikiwa imesalia pekee ikichuana na watetezi Yanga katika kuwania ubingwa tofauti na ilivyodhaniwa mwanzoni na mashabiki.


Kocha huyo amewapa dakika 90 mastaa wa timu hiyo akiwamo kinara wa mabao Jean Charles Ahoua, Ellie Mpanzu na Steven Mukwala kumalizana kwanza na Kagera Sugar kesho katika mechi ya Ligi Kuu kisha ndipo waanze mipango ya pambano la dabi la Juni 25.

Simba itakuwa wenyeji wa Kagera iliyoshuka daraja kwenye Uwanja wa KMC Complex, uliopo Mwenge, Dar es Salaam, ikisaka pointi tatu zitakazoiweka pazuri kuwania ubingwa mbele ya Yanga Jumatano ijayo kombe likiwa uwanjani na Fadlu amewawashia moto mastaa wa timu.

Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti jana kuwa, licha ya ushindi wa mabao 5-0 walioupata dhidi ya KenGold katika mechi iliyopita, anataka kuona washambuliaji wa timu hiyo wakiwa na wastani mzuri zaidi wa utumiaji nafasi hasa katika mechi mbili zilizosalia dhidi ya Kagera na Yanga.

“Tuna nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi, ndio kitu kilicho mbele yetu kwa sasa, hivyo tunatakiwa kuongeza umakini katika mechi hizi ambazo zimesalia kuanzia katika utumiaji nafasi hadi katika namna ya kujilinda,” alisema Fadlu. Katika mechi dhidi ya KenGold, Simba ilitengeneza nafasi nyingi, lakini ilizipoteza zikiwemo alizopata Ahoua, licha ya kufunga bao moja, alikosa nafasi tatu wazi ambazo zingeongeza idadi ya mabao.

Fadlu alisisitiza Kagera siyo ya kubeza hata kidogo, kwani haina presha ya kusaka matokeo kutokana na kushuka daraja mapema.

Alisema timu ambazo tayari zimeshuka hucheza kwa uhuru zaidi.