Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michuano ya U20 Morogoro yaiponza Mbuyuni Academy

Michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wilaya ya Morogoro 2022, imeiponza timu ya Mbuyuni Academy baada ya kushindwa kufika kituoni katika michezo ya michuano hiyo dhidi ya Motasoa Academy na kuambulia adhabu kali kwa mujibu wa kanuni mkoani hapa.

Michezo ya michuano ya vijana chini ya umri huo inafanyika katika uwanja wa Sabasaba mkoani hapa ambapo Mbuyuni imejikuta ikipata dhabu kutoka kamati ya mashindano hayo.

Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa, Katibu wa chama cha soka wilaya ya Morogoro (MDFA), Geofrey Mwatesa amesema Kamati ya mashindano ya vijana U20 imeifungia timu ya Mbuyuni kutoshiriki mashindano yoyote ndani na nje ya wilaya kwa muda wa miaka mitatu na kutakiwa kulipa faini ya sh250,000 kutokana na kutofika kituo siku ya mchezo wao namba 39 dhidi ya Motasoa academyMbuyuni Academy.

Mwatesa amesema kutokana na adhabu hiyo Mbuyuni Academy imepoteza ushindi na timu pinzani itapata ushindi wa pointi tatu na magoli matatu huku kiongozi yoyote amefungiwa kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, itaondolewa katika mashindano na inaweza ikakabiliwa na adhabu zaidi kama ambavyo chama cha mpira wa miguu cha wilaya kitaona inafaa.

“Adhabu hii imeanza mara moja kwa Mbuyuni Academy kutumikia baada ya kushindwa kufika kituoni kucheza na wapinzani wao Motasoa Academy na hii ni kutokana na kanuni zinazotumika katika michuano hii ni ile ya TFF.”amesema Mwatesa.

Kwa upande wa Katibu wa timu ya vijana ya Mbuyuni Academy ya Misongeni, Abeil Palanjo amesema wamepokea taarifa za adhabu hiyo kwa masikitiko kutokana lengo la vijana hao kuonyesha vipaji vya soka katika mashindano hayo.

“Kocha mkuu na mimi kama Katibu tulipata dharura ya kusafiri nje ya Morogoro na tuliowaachia majukumu wamefanya uzembe wa kushindwa kuipeleka timu katika kituo na hii imetuathiri kwa kiasi kikubwa adhabu hii.”amesema Palanjo.

Palanjo amesema katika michezo ambayo wamecheza wameshuka dimbani mara mbili na kupoteza zote ikiwa katika mchezo wa kwanza wakipoteza kwa kipigo cha bao 4-1 ddhidi ya Mafisa United huku wakipoteza mchezo mwingine mbele ya Pwani Sports Foundation kwa bao 2-1.

“Mchezo wetu na Motasoa Academy vijana wetu walikuwa na morari ya juu kutaka kupata ushindi lakini majukumu ambayo tuliyaacha kwa viongozi wenzetu hayakufanyiwa kazi na hii inarudisha nyuma juhudi za kuendelea kuibua na kuendeleza vipaji.”amesema Palanjo.