Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgeveke: Mayele mh!

BEKI wa kati wa Dodoma Jiji, Joram Mgeveke amesema straika wa Yanga, Fiston Mayele ni mtu kweli kweli ila anafurahi kufanikiwa kumkaba asifunge bao wakati Yanga ikishinda mabao 2-0.

Mayele katika mchezo huo alicheza kwa dakika 88 kabla ya kumpisha Heritier Makambo ikiwa ni mechi yake ya nne mfululizo bila kufunga bao.

Mgeveke kwa kushirikiana na Salmin Hoza pamoja na Augustino Nsata walimdhibiti Mayele asifunge lakini baada ya mechi hiyo akatamba kwamba ana mechi sita amesaliwa nazo atatetema tu.

Mgeveke ambaye amewahi kuzichezea timu za Simba na Mwadui alisema alijifungia chumbani na kuangalia uchezaji wa Mayele na kugundua hatakiwi kupewa nafasi ya kupiga golini kwani ana uwezo mkubwa wa kutumia nafasi.

“Nilimsoma jinsi ya kumkaba ili asifunge na akituliza unatakiwa kuingia uvunguni ili kumpoteza mwelekeo, kikubwa ni kwamba kuna mechi kadhaa nilikosa nikawa naangalia uchezaji wake, Mayele sio mtu wa kumwachia nafasi,” alisema na kuongeza; “Kocha aliangalia zile sehemu za hatari za Yanga na kututaka kuziba tulifanikiwa Mayele asifunge ila bahati mbaya tulipoteza mchezo.”